Na
Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dk Ibrahimu Msengi ameziagiza Taasisi za
Serikali zilizopo katika Mkoa wa Katavi ameziagiza
zihakikishe zinalipa madeni yao makubwa na yamuda mrefu
wanayodaiwa na Mamlaka ya Maji safi na maji taka ya mji wa Mpanda
(MUWASA) ili mamlaka hiyo iweze kujiendesha
Agizo hilo
alili maadhimisho ya kilele cha cha maadhimisho ya
wiki ya maji yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Ngoma lusambo
Wilaya ya Mpanda katika hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Kaimu mkuu
wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele
Kanali msitaafu Issa Njiku
Alisema
mamlaka ya maji safi na maji taka ya mji wa Mpanda imekuwa ikikwama kujiendesha
kufanya baadhi ya shughuli zake kutokana na madeni makubwa ya
fedha ambayo MUWASA wanazidai baadhi ya Taasisi
za Serikali zilizopo katika Mkoa wa Katavi kwa muda mrefu sasa na huku
wakiendelea kupatiwa huduma ya maji
Alifafanua
ili Mamlaka hiyo ifanye shughuli zake vizuri taasisi
zote zote ambazo zinadaiwa madeni makubwa ziakikishe zinalipa
madeni hayo haraka kwa MUWASA ili mamlaka hiyo iweze
kujiendesha
Aliitaka
mamlaka ya maji safi na maji taka ya Mji wa Mpanda kuwa na
utaratibu wa kugawa maji kwa wananchi kwa uangalifu na
bila kuwa na upendeleo wowote kwa wateja wao
Alitowa
wito kwa mamlaka zinazosimamia maji ziweke mpango wa
kuwapatia wananchi maji safi na salama kwa gharama
nafuu
Dk
Msengi alisema kamati za maji ziundwe kwenye kila Kijiji na
mtaa ili kamati hizo zifanye kazi ya kusimamia maji
kwenye vijiji vyao na mitaa yao
Alisema
kazi ya usambazaji wa maji unaendelea
vizuri kwani asilimia kubwa ya wananchi wa
Mji wa Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wanapata maji safi na
salama
Katika
maadhimisho hayo ya wiki ya maji kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Kanali
Mstaafu Issa Njiku alizindua mradi wa maji katika Kijiji cha Ngoma
Lusambo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 288 ulifadhiliwa na
Benki ya Dunia maradi huo ambao utawasaidia zaidi ya wakazi 2000 wa
kijiji hicho
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment