Katavi
Watu watatu wamekufa hapohapo na wawili wamejeruhiwa na kulazwa Hospitalini baada ya Roli walilokuwa wanasafilia kupinduka katika Mlima Kalutwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi
Ajari hiyo ambayoililihusisha Roli aina ya Scania yenye Namba za usajiri T.211 AGF lililokuwa likiendeshwa na Dreva aliyejulikana kwa jina moja la Amri ilitokea hapo jana majira ya saa moja usiku katika mlima wa Kalitwa barabara ya kutoka Mpanda kwenda Mkoa wa Kigoma
Kamanda Kidavashari alisema mpaka sasa kati ya marehemu hao watatu ameweza kutambulika marehemu mmoja aliyetambulika kwa jina la Edrick Ndigimiti (MASABO) 30 Mkazi wa Kigoma
Kwa mujibu wa Kidavashari miili ya marehemu hao ipo katika chumba cha kuifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Alisema huhudi za kuwatambua marehemu hao wawili ambao bado hawajatambulika zinaendelea kufanyika kwa kuwatafuta ndugu zao
Kamanda Kidavashari aliwaja majeruhi wawili wa ajari hiyo kuwa ni Dickison Mwangalonga (19)Mkazi wa Mtaa wa Kotazi mjini hapa ambae ameumia katika sehemu za usoni na mkono wa kushoto na Mohamed Usoni Mkazi wa Mtaa wa Majengo Mjini hapa ambae ameumia mguu wa kulia mkono wa kushoto na mgongoni
Alisema majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na wanaendelea kupatiwa matibabu zaidi na hari zao zinaendeleavizuri
Kwa mujibu wa Kidavashari chanzo cha ajari hiyo kilitokana na mwendo kasi wa Dreva ambapo mara baada ya kutokea kwa ajari hiyo kutokea alikimbia kusiko julikana
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kuhakikisha linamkamata mtuhumiwa wa ajari hiyo ili achukuliwe hatua za Kisheria
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment