Na
Walter Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi limemkamata na linamshikilia Kulwa
Rajabu (35) Mkazi wa Mtaa wa Kashaulili Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma
za kumkamata na viungo vinavyosadikiwa kuwa ni vya Binadamu na
nyara za Serikali
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi mwandamizi
Dhahiri Kidavashari mtuhumiwa huyo alikamatwa na viungo hivyo na nyara za
Serikali hapo jana majira ya saa tatu usiku
nyumbani kwake katika Mtaa wa Kashaulili mjini hapa
Alisema
mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa ambazo zilikuwa zimelifikia
jeshi la Polisi kutoka kwa Raia wema ambao walitowa taarifa
kwa polisi kuwa mtuhumiwa ameifadhi viungo vya binadamu na nyara za
Serikali ndani ya nyumba yake
Alifafanua
baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi walianza kufanya
uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo zilizokuwa zikimkabili Kulwa
Rajabu
Kamanda
Kidavashari alieleza ndipo hapo jana Polisi walipokwenda
nyumbani kwa mshitakiwa na walipofika nyumbani kwake walimfanyia upekuzi
huku wakiwa na viongozi wa Mtaa huo
Alisema
katika upekuzi huo Polisi walifanikiwa kumkamata mshitakiwa akiwa
amehifadhi ndani ya nyumba yake mifupa mitatu ,mshipa mmoja
wa chini ya kinena unaodhaniwa ni wa mtu mwanaume na meno
mawili viungo hivyo vinadhaniwa ni vya Binadamu
Kidavashari
alisema mbali ya mtuhumiwa kukamatwa na viungo hivyo pia mtuhumiwa
huyo alikamatwa akiwa amehifadhi ndani ya nyumba yake nyara za Serikali
Alizitaja
nyara alizokamatwa nazo mtuhumiwa Kulwa Rajabu kuwa ni
kipande cha ngozi ya Kalungu yeye na singa mbili
za Tembo
Kamanda
Kidavashari alisema mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani ili
akajibu mashitaka mawili ya kupatikana na viungo vinavyosadikiwa
kuwa ni vya Binadamu na kupatikana na nyara za Serikali
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment