Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Alson
Kibona (17) mwanafunzi wa kidato
cha nne shule ya Sekondari Nsemlwa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameuwawa baada ya kupigwa kichwani na
mpini wa koleo na nasehemu
mbalimbaliza mwili wake na baba yake
mzazi kwa kosa la kutokwenda
shuleni
Kaimu kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa
Katavi Rahid Mohamed alimtaja
mzazi anayetuhumiwa kumuuwa
mwanae kwa kumpiga na mpini wa
koleo kuwa ni John Kibona(35) mkazi wa
mtaa wa Nsemlwa Mjini hapa
Alisema tukio hilo hilo la mauwaji ya mwanafunzi lilitokea hapo juzi majira ya saa tisa
usiku nyumbani kwa mtuhumiwa
katika mtaa wa Nsemlwa
Kwa
mujibu wa Rashid Mohamed Siku
hiyo ya tukio marehemu Alson alikuwa amelala chumbani
mwake ndipo baba yake alipomwamusha na kuanza kumuoji kwanini amekuwa na tabia ya utoro wa mara kwa mara wa kutokwenda shuleni
Mohamed alisema
ndipo mtuhumiwa alianza kumpiga marehemu kwa kutumia
mpini wa koleo kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake
huku akiwa akimkanya kwa maneno kuwa
aache tabia ya utoro wa shuleni
Alisema marehemu baada ya kuona kupigo kimemzidia alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada hata hivyo mtuhumiwa hakujali aliendelea kwa
kumpa kichapo mwanae huyo
Siku iliyofuata marehemu aliaka huku
akiwa na maumivu makali katika sehemu mbalimbali za mwili wake hari
ambayo ilimlazimu ashindwe hata kwenda shule
na mthumiwa hakujali wala
kumpeleka kwenye matibabu
Kaimu
Kamanda Rashid Mohamed
alieleza siku hiyo ilipotimia majira ya saa sita marehemu
alikwenda kisimani kuteka maji ya kuoga
ambapo alipoinama iliachote maji
damu zilianza kumtoka mdomoni
na puani na kisha kuanguka chini pembezoni mwa kisima hicho
Alisema
majirani waliokuwa karibu na eneo hilo walimchukua marehemu
na kumpeleka katika Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya kupatiwa
matibabu
Alifafanua
wakati akiwa anaendelea kupatiwa
matibabu katika Hospitali hiyo alifariki
Dunia kutokana na majeraha makubwa aliyokuwa ameyapata kutokana
na kipigo alichokuwa amekuwa
amekipata
Baada
ya mthumiwa kupata taarifa kuwa mwanae
amepelekwa Hospitali na wakati
akiwa anapatiwa matibabu amefariki
Dunia aliamua kutoweka
na kukimbilia sehemu kusiko julikana
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Katavi alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na ndugu wa
marehemu na uongozi wa mtaa linamsaka
mtuhumiwa ili kumkamata
na aweze kujibu tuhuma inayomkabili
Aidha kaimu
kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi ametowa wito
kwa wazazi na walezi kuacha tabia
ya kutumia nguvu kwa kuwapiga watoto wao na badala yake wawaelimishe
na kuwaeleza umuhimu wa elimu
ili kuepuka matukio mbaya
ya nanma hii ndani ya jamii
MWISHO
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment