Home » » TUKIO LA KUTISHA NA KUSIKITISHA: MWENYEKITI WA KITONGOJI ACHINJWA SHINGO AKAKATWA VIUNGO VYAKE VYA MWILI NA KUPIKWA KWENYE SAFURIA, SOMA HAPA TAARIFA

TUKIO LA KUTISHA NA KUSIKITISHA: MWENYEKITI WA KITONGOJI ACHINJWA SHINGO AKAKATWA VIUNGO VYAKE VYA MWILI NA KUPIKWA KWENYE SAFURIA, SOMA HAPA TAARIFA


N a  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mwenyekiti  wa Kitongoji    cha  Songambele Kata ya Ilela Tarafa  Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  (ACT) Richald Madirisha(31) ameuwa kikatili kwa kuchinjwa  shingo  na kutenganishwa na  kiwiliwili chake na kisha nyonfolewa  viungo vyake vya mikono na miguu na  sehemu zake za siri  na kisha  kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  mauwaji hayo ya kikatili na  kutisha  yalitokea hapo jana majira ya saa tano na nusu usiku nyumbani kwa marehemu
 Siku hiyo hiyi ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe  aitwaye  Mekilina  Mussa  ghafla walitokea watu watano ambao  hawafahamiki na  kuvunja mlango kisha waliingia ndani ya nyumba
 Kamanda Kidavashari alisema  watu hao ambao walikuwa wameshika mapanga  baada ya kuingia ndani ya nyumba waliingia chumbani kwa marehemu  na kumlazisha mkewe ajifishe kwa kujifunika na shuka usoni na alale kitandani
 Alisema  baada ya mkewe kujifunika na shoka usoni watu hao walianza kumchinja shingo mrehemu  kwa  kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu alivyo kuwa  akilia kwa uchungu
 Kidavashari alieleza baada ya kuwa wamemchinja shingo  walichukua kichwa chake na kukiweka kwenye safuria na kuweka maji ndani ya safuria na kutoka nacho nje na  kupipika  kwenye moto ambao ulikuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu
 Alisema kisha watu hao walirudi ndani ya nyumba na kunyomfoa sehemu za siri za marehemu na mikono yake  na kwato za miguu  kisha  waliziweka kwenye  safuria  jingine  na  kuvipika  kwenye moto
Kisha watu hao  waliondoka  na kutokomea kusiko  julikana huku wakiwa wameviacha  viongo hivyo vya marehemu vikiwa vinaendelea kuchemka  ndani ya safuria hizo
 Kidavashari alisema  mke  wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo  na kukuta viongo hivyo vikiwa  ninaendelea kuchemke  kwenye safuria hizo huku kiwailiwili chake kikiwa ndani ya chumba chake
 Amesema uchunguzi wa  awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji  kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora  ambae  alikuwa akimtuhumu marehemu  kuwa amemnyanya  mwanamke ambae walikuwa  na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua   kuhama nae kijijini  hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele  Wilaya Mlele
 Kamanda Kidavashari  alieleza   jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia  watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya kikatili


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa