Home » » RC MARUFUKU KUFUNGUA MIRADI ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

RC MARUFUKU KUFUNGUA MIRADI ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dr Ibrahimu Msengi  ameiPINGA  marufuku Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  kumwalika  yeye  kutembelea na kukagu miradi yote ya  maendeleo iliyojengwa chini ya  kiwango  kwani hayuko tayari  kufungua miradi yote ya maendeleo iliyojengwa chinii ya kiwango
 Rc alitowa kauli hiyo hapo jana  wakati wa ziara yake ya  kukagua  maendeleo ya ujenzi wa  majengo ya maabara ya shule za Sekondari za  Ikola na Karema zilizoko katika Tarafa ya Karema  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  baada ya kutoridhishwa na  ujenzi wa  majengo ya maabara katika Sekondari ya Ikola  
Alisema  miradi mingi ya ujenzi wa  majengo ya Halmashauri  inajengwa chini ya kiwango kutokana na kutokuwa na usimamizi wa wataalamu wa kutoka kwenye Halmashauri husika
 Alisema yeye kama Mkuu wa Mkoa hata kubali  kungua jengo lolote katika Mkoa wa Katavi ambalo  limejengwa  chini ya kiwango na wala Halmashauri isimwalike kutembelea miradi ya namna hiyo  na hata kubali lifunguliwe
 Alifafanua kuwa  ni aibu kwa karne ya leo   majengo kujengwa chini ya kiwango wakati huo ambao  kuna   zana za kisasa  bora  zaidi  kuliko wakati wa zamani
 Dr  Msengi  alisema inashangaza sana kuona majengo ya watu  binafsi yanajengwa kwenye kiwango kizuri huku majengo ya sekari yakiwa yanajengwa chini ya kiwango kwani hao watu binafsi  wakati mafundi ni walewale  alihoji i RC
 Alieleza  swala la ujenzi wa  majengo ya maabara  sio la mzaha  endapo kutatokea na kiongozi yoyote katika mkoa wake atakae zembea atahakikisha anamwajibisha
 Dr Msengi  alisema yeye   taarifa  za kusomewa kwenye makaratasi  azimsumbui  kwani  utaratibu wake ni lazima afike kwenye eneo husika  na akikuta kuna tatizo lolote atamwagiza  mkandarsi  aliyejenga  jengo alivunje  na kisha  alijenge kwa gharama zake
 Kauli hiyo aliitowa baada ya kutolidhika na ujenzi  wa jengo  ya vyumba vitatu vya maabara vya shule ya  sekondai ya Ikola  hari ambayo ilimlazimu amwangize mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kuhakikisha milango yote iliwekwa kwenye majengo hayo inaondolewa na kuwekwa mingine yenye ubora kwa gharama za mkandarasi aliyejenga majengo hayo
 Pia  amewaagiza  Wakurugenzi wote wa Halmashari za Mkoa wa Katavi  kuhakikisha kila jengo linalojengwa  kwenye Halmashauri zao  linapangiwa na mtaalamu wa kulisimamia  na awe anasaini  kitabu kila atua anayokuwa anakagua  na ratiba hiyo  wawe nayo wakarugenzi ofisini mwao
 Aidha aliwataka walimu wa shule za misingi na Sekondari kuwa kusimia kwa karibu majengo ya madarasa , nyumba za waalimi pamoja na matundu ya choo yanayojengwa kwenye shule zao na pale wanapoona majengo hayo yanajengwa chini ya kiwango watoe taarifa kwa viongozi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa