Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dr Ibrahimu Msengi
amewaagiza watu wote waliovamia
kwenye maeneo ya vyanzo vya maji
na hifadhi za mistu na kingo za mito
waondoke kwa hiari kabla ya Serikali haija waondoa kwa nguvu kwenye maeneo hayo
Rc Dr Msengi
alitowaagizo hilo hapo jana
kwenye siku ya upandaji miti kimkoa wa Katavi iliofanyika kimkoa kwenye Tarafa ya Mwese Wilaya ya
Mpanda wakati alipokuwa akiwatutubia
Wananchi
Alisema hari ya
hari ya uharibifu wa mazingira
katika Mkoa wa Katavi imekuwa
ikiongezeka siku hadi siku huku wananchi na viongozi wa maeneo hayo wakiwawanaona kama ni jambo la kawaida
Alieleza
kuwa kila mtu anahaki na wajibu
wa kuhakikisha anatunza mazingira
na Sesrikali ya Mkoa wa Katavi haita kuwa na huruma
kwa mtu yoyote ambae atakae patikana anaharibu
mazingira hivyo watu wote wanaoishi kwenye vyanzo vya maji na hifadhi za mistu na kwenye kingo za mito
waanze kuondoka kwa hiari kabla ya Serikali haija waondoa kwa nguvu kwani jambo
la kuwaondoa halitakuwa na mjadala tena
Alifafanua
wapo baadhi ya watendaji wa
vijiji na Kata wamekuwa wakiwaonea watu aibu
na kuwaogopa na kuwaacha wakiangusha miti ovyo bila utaratibu
huku viongozi hao wakiwepo kwenye maeneo hayo
Alisema kuanzia sasa mtendaji wa Kijiji na Kata ambae kutatokea uharibifu wa mazingira kwenye eneo
lake atawajibishwa yeye
kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake
RC Msengi alisema hari ya
uharibifu wa mazibgira imekuwa
ni kubwa sana katika Mkoa wa Katavi na tayari hari hiyo
imeanza kusababisha upungufu wa mvua katika Mkoa huu kwani mvua zinazonyesha
kwa sasa hazilingani na mvua zilizokuwa zikinyesha miaka ya nyuma kabla ya
mazingira yalipo kuwa hajaharibiwa na watu
Alisema
wakulima na wafugaji waitwe
na waelezwe na viongozi wa kwenye maeneo
yao sheria za utunzaji wa mazingira zilivyo ili Serikali inapowachukulia hatua wasione
kuwa wameonewa
Alifafanua kuwa
lengo la Serikali ya Mkoa wa Katavi sio kuwafukuza wafugaji na wakulima bali ni kuhakikisha mzingira yanatunzwa
vizuri na watu hawakati miti ovyo
Alisema Halmashauri za Mkoa wa zote zilizopo
katika Mkoa wa Katavi zianze
kuangalia utaribu wa namna
ya kuzuia watu wasikate miti
ovyo na
kila mti unaokatwa uwe unajulikana unakatwa kwanini na kwa matumizi yapi
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda Estomiel Chang’ah alisema zoezi
la kuwahamisha watu wanaoishi kwenye vyanzo vya maji na hifadhi za mistu na
kuharibu mazingira limekuwa likikwamishwa na viongozi wa siasa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment