Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr
Ibrahimu Msengi amewaagiza
wanafunzi wote wa Sekondari ya Mwese Wilaya ya Mpanda walioacha
kuendelea na masoma kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo ushirikina na kuolewa warudi sheleni na waendelee na masomo yao
Mkuu huyo wa Mkoa Dr Msengi alitowa agizo hilo hapo juzi
wakati wa kikao chake na waalimu wa shule ya Sekondari ya Mwese kilichofanyika
shuleni hapo
Agizo hilo alilitowa kufuatia taarifa iliyotolewa mbele yake
na mkuu wa shule hiyo mwalimu Yohana Manyanda ambae alieleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na
tatizo kubwa la utoro wa wanafunzi na
kupelekea mabweni ya shule hiyo kuwa wazi
Alisema shule hiyo
inayomabweni yanayoweza kutumiwa na wanafunzi wasichana 100 lakini
wanafunzi wanaotumia mabweni hayo mawili ni wanafunzi saba na bweni moja la wanafunzi wavulana lililiopo
shuleni hapo lenye uwezo wa kutumiwa na
na wavulana 50 linatumiwa na wanafunzi 13 tuu
Mkuu huyo wa shule
alieleza kuwa utoro wa wanafunzi wa sekondari hiyo yenye
jumla ya wanafunzi 187 wavulana
85 na wasichana 102 unatokana na sababu mbalimbali zinazochangiwa na wazazi wao kuwa na imani za
kishirikiana ambao wanaamini kuwa watoto wao wakiwa shuleni
wataugua ugonjwa wa kuanguka na wengine wameacha masomo na kuolewa
Kufuatia taarifa kutolewa mbele yake Mkuu wa Mkoa Dr Msengi alisema Serikali haiko tayari kuona wanafunzi hao wa shule hiyo
wanaacha kuendelea na masomo kwa sababu zisizo na msingi
Alisema nawaagiza wanafunzi wote ambao walioacha masomo
kwenye shule hiyo warejee shuleni na
baada ya mwezi mmoja masako mkali utafanyika kuwasaka na kuwarejesha
kwa nguvu wanafunzi wote ambao watakuwa wameshindwa kurejea shuleni na wazazi
wao nao watafikishwa mahakamani
Niabu kusikia
wanafunzi wanashindwa kusoma shele huku mabweni ya wanafunzi yakiwa wazi
wakati maeneo mangine ya Nchi wanalilia shule zao kuwa na mabweni
Alisema agizo lake
hilo si lamzaha na litaendelea pia kwa maeneo yote ya Mkoa wa Katavi na
wazazi wa wanafunzi watakao bainika watoto wao wameacha masoma watachuliwa
hatua za kisheria kwani taratibu za sheria za kuwashitaki wazazi wao zipo wazi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment