Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Baadhi ya Walimu wa shule za Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda wanalazimika kuruhusu wanafunzi wanaonyonyesha kuacha masomo na kuruhusu kurudi nyumbani kwao kwenda kunyonyesha watoto
Mamalamiko hayo ya baadhi ya waalimu yalitolewa hapo jana na waalimu hao kwenye mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Mtakatifu Maria mjini hapa
Waalimu hao walisema wamekuwa wakilazika kuwaruhusu wanafunzi wanaowafundisha kuacha vipindi vya masomo darasani na kuwaruhusu warudi nyumbani kuwanyonyesha watoto wao nyumbani pindi wanapokuwa wameomba ruhusa hiyo
Mmoja wa waalimu wa shele ya Sekondari Nsemlwa mwalimu Zakaria Leonald alisema yeye huwa analazimika kumpatia ruhusa mwanafunzi mmoja ambae huwa anakuja shuleni huku akiwa amemuacha mtoto anae nyonya nyumbani
Alisema mwanafunzi huyo huwa anakuwa analalamika darasani wakati vipindi vinapokuwa vinaendelea kuwa maziwa yake yanamuuma kwa kuwa yanakuwa yamejaa kutokana na kuto na kuwa yamejaa kutokana na kutomnyonyesha mtoto wake kwa muda mrefu
Alisema hali hiyo ya kuwachannnnnnnnganya wanafunzi ambao waliozaa na ambao hawaja zaa imekuwa ikiwaathili baadhi ya wanafunzi wa wasichana
Alifafanua kuwa serikali iangalie utaratibu wa kuwa na shule maalumu kwa ajiri ya wanafunzi wale ambao wananyonyesha kama ambavyo inavyofanyika kwa shule zenye mahitaji maalumu kauli hiyo ambayo iliungwa mkono na waalimu wengi kwenye mkutano huo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment