Home » » SERIKALI KUWAPATIA RUZUKU WAVUVI WA SAMAKI

SERIKALI KUWAPATIA RUZUKU WAVUVI WA SAMAKI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Serikali imepanga  kutoa ruzuku kwa wavuvi wa samaki ili kuwawezesha wavuvi waweze  kupata  vyombo  bora vya uvuvi vitakavyowasaidia  kwa ajiri ya shughuli zao za uvuvi  ili weweze   kununua zana bora  ili  waondokane na uvuvi wa zana duni za uvuvi
 Hayo yalisemwa hapo jana na Waziri wa Maendeleo Mifugo na uvuvi Dr Titus   Kamani   wakati  alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ikola   wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua miradi mbalimbali  inafanywa  na Wizara hiyo Mkoani hapa
DR  Kamani  alisema  Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya uvuvi  imeamua  kuanza kutowa  ruzuku kwa wavuvi  kama ambavyo inavyofanya  kwa wazalishaji wa mazao  mbaalimbali ya kilimo
 Alifafanua  shughuli za uvuvi  zimekuwa ni tegemewa na watu wengi kwa ajiri ya kujipatia kipato chao  ambapo  jumla ya watu zaidi ya milioni nne  wanajishughulisha na  uvuvi  na kuwa ndio sehemu yao ya kujipatia kipato chao na ajira
 Alisema  Serikali inatambua  kuwa wananchi  hawajanufaika  na kufaidika  na uvuvi  kutokana na kuendelea kutumia  zana  duni  kwenye  shughuli zao za uvuvi
 Dr  Kamani alieleza katika kuhakikisha sekta ya uvuvi inaendelea kukua hapa nchini Serikali  imeongeza   vyuo vya wataalamu wa samaki  ili Serikali  iweze kuwa na  wataalamu maalumu kwa ajiri ya  samaki tuu
 Aliwata wavuvi wa samaki  waanze kuwa na utaratibu wa  kujiunga  na mifuko ya hifadhi ya jamiii  ambayo itawakopesha  na kuwafanya  waweze kununua zana bora za uvuvi na pia waweze kujiwekea akiba yao ya uzeeni kwani   watakuwa wamejiwekea akiba yao pindi watakapo kuwa wamezeeka
 Kwa hari hiyo  maafisa ushirika wafike kwenye maeneo ya wavuvi na kuwaelimisha namna ya kuunda vikundi vya ushirika  ambavyo vitawasaidia  kukopa kwenye mifuko ya  kijamii
Kwa upande  Katibu  Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Emanuel Kalobelo  alisema  wavuvi wa samaki wa Mkoa wa  Katavi wamefanikiwa  kuongeza  matumizi ya zana bora za  uvuvi  kutoka  boti  za injini  290 julai   2013 hadi  boti za  injini  385 Desemba  2014 sawa na ongezeko la asilimia 25
Aidha   Mkoa wa Katavi  umetowa mafunzo  ya elimu ya   uvuvi  kwa wavuvi  2,420 kwa mwaka 2014 yatakayowasaidia  kupata maarifa ya uvuvi ukilinganisha na  mwaka 2013 ambapo wamafunzo yalitolewa kwa wavuvi  812
 Mwandisi Kalobelo alisema Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  kwa mwaka wa fedha wa 2014 na 2015 imetenga kiasi cha shilingi milioni 40 imetenga kwa ajiri ya  kununua boti  za uvuvi  ambapo hadi sasa  injini mbili  aina ya  Yamaha  zenye ukubwa  wa  40 HP   zimenunuliwa
Alisema  ni matarajio ya Mkoa  kuwa  uwepo wa  boti  hizo utapunguza  kwa kiasi  kikubwa uwepo wa  uvuvi haramu  katika Ziwa Tanganyika
 Alifafanua  Mkoa wa Katavi  katika  kutekeleza  sera  na  mkakati  wa Taifa wa sekta ya uvuvi  ya mwaka 1997 pamoja  na sera  ya uvuvi   ya mwaka 2003 umehamasisha  wananchi  kufuga samaki  ili kuboresha  afya  na kupunguza  umasikini  wa kipato
 Alisema  hadi kufikia desemba mwaka jana  mkoa wa Katavi  ulikuwa  na jumla ya mabwawa  hai 60  ya kufungia samaki  yalioanzishwa  na wafugaji binafsi  ukilinganishwa  na mabwawa  51 ya mwaka 1013 hili ni sawa na ongezeko la asilimia 15
 Alieleza  pamoja na  ongezeko hilo  Mkoa  unakabiliwa  na changamoto  ya kukosekana kwa kituo cha kuzalisha  mbegu  bora   za   vifaranga  vya samaki  jambo  lililosababisha   wafugaji wengi  kushinnnnnnnnndwa kupata  mbegu bora  ya samaki
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa