Home » » MARUFUKU KUFANYA MINADA YA MIFUGO BILA KUWEPO MIZANI

MARUFUKU KUFANYA MINADA YA MIFUGO BILA KUWEPO MIZANI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Wiara ya Mifugo na imeziagiza Halmashauri zote hapa ncini  kuacha mara moja  kufanya  minada ya mifugo kwenye minada yote  ya kuuza  mifugo ambayo  haina mizani ya kupimia mifugo
Agizo hilo  limetolewa hapo jana na Waziri wa  Maendeleo  ya mifugo  na uvuvi  Dr  Titus  Kamani   wakati   alipokuwa  akizungumza  na viongozi wa Mkoa wa Katavi  na wafugaji na  pamoja  na  wavuvi katika  katika ukumbi  wa  ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi
 Alisema  wafugaji wamekuwa  hawanufaiki na mifugo yao wanayoiuza  kutokana  na kuuza  mifugo  yao  bila kupimwa  kwenye  mizani kutokana na  maeneo mengi ya minada inayomilikiwa na Halmashauri kutokuwa na  na mizani ya kupimia   uzito wa mifugo
 Dr  alieleza  Serikali imeagiza kuanzia sasa  maeneoo yote ya minada  yawe na mizani ya  kupimia mifugo  ilikumfanya mfugaji afahamu uzito wa mifugo yake  inauzito wa kiasi gani na aweze  kuuza  kulingana na hari halisi ya uzito  wa  mifugo yake na kumfanya mfugaji  anufaike
 Alifafanua  kuwa  mazao  mengine  yote  yanayouzwa kwenye  minada hapa nchini   wafanyabiashara  uuza zao yao  yote  hupimwa  kwa mizani  kwanini na mifugo nayo isipimwe kwenye mizani alisema Waziri  Kamani
 Alisema hari hiyo ya  wafugaji  kutouza  mifugo yao  kwa kupima  kwenye mizani  kumewafanya baadhi ya  wafugaji wengine  kukata tamaa  ya kujishughulisha na maswala ya ufugaji wa mifugo
 Katibu   Tawala wa Mkoa wa Katavi  katika taarifa aliyoisoma  ya sekta ya mifugo alieleza kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya Ng’ombe  244,009 mbuzi  120,000   kondoo 43,358 hata hivyo ufugaji  huo  wa mifugo  haufanyiki  kisasa  kwa hari hiyo Mkoa  unalo jukumu  hili  la kuendeleza  sekta ya mifugo
Alisema  mkoa umetowa mafunzo kwa wafugaji     4,591kwa kipindi cha mwaka  2013 na mwaka 2014  ambao wamepatiwa  mafunzo  juu ya ufugaji  bora wa ng’ombe  wa maziwa na nyama  vikundi vitatu  vimepata mafunzo ya uchakataji  wa ngozi  wafugaji 10 wamepatiwa  mafunzo ya  uendeshaji wa ranchi  katika Ranchi ya Kalambo Mkoani Rukwa  na wafugaji  215 wamepata mafunzo ya ufugaji  bora wa  kuku  wa asili
 Mwandisi Kalobelo alieleza Mkoa wa Katavi unakabiliwa na changamoto  ya upungufu wa  wataalamu wa  mifugo ambapo kwa sasa inao wataalamu 27 wakati wanaohitajika ni wataalamu  67 hivyo kuna  upungufu wa wataalamu 40 wa mifugo katika Mkoa huu
 Alitaja changamoto nyingine kuwa ni  uhaba  wa vitendea kazi  kama vile vyombo  vya usafiri  magari ,pikipiki  kwa ajili ya  matumizi ya  shughuli za  kiutendaji  wa sekta hiyo ya Mifugo katika mkoa wa Katavi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa