Home » » HALMASHAURI MPANDA KUNUNUA MITAMBO YA KUTENGENEZEA BARABARA YA ZAIDI YA BILIONI MOJA

HALMASHAURI MPANDA KUNUNUA MITAMBO YA KUTENGENEZEA BARABARA YA ZAIDI YA BILIONI MOJA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi  imepanga kununua  mitambo ya kutengenezea barabara  yenye thamani ya Dola za Kimarekani 676,240 sawa na fedha za kitanzania kiasi cha  shilingi  bilioni 1,149,608,000
Uamuzi wa kununua mitambo hiyo ya kutengenezea barabara ulipishwa hapo jana     kwenye baraza maaalumu la  madiwani la  Halmashauri hiyo lililofanyika jana kwenye ukumbi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  uliopo mjini  hapa
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Estomikh Chang’ah  alilieleza  baraza hilo la madiwani  kuwa fedha za kununulia mitambo hiyo  zimepatikana  kufutia Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kuPATIWA  mkopo wa fedha kutoka Benki ya TIB  za kununulia mitambo hiyo
 Alisema katika ununuzi huo wa mitambo  hiyo Halmashauri  inatakiwa kulipa kwanza   ndani ya siku  21   wawe wamelipa  kiasi cha Tsh 230,000,000 kwenye Benki ya TIB   mkopo  huo  ni  wakipindi cha cha miaka mitano
Chan’gah aliitaja mitambi hiyo itakayo nunuliwa kuwa ni  Greda  Made 149K  litakalogharimu kiasi cha  dola za Marekani  436,600 sawa na Tsh milioni  742,200,000 na kijiko Model 320DL kwa gharama ya dola  233,640 sawa na fedha Tsh  milioni 397,188,000 na gharama za kusafirishia  mitambo hiyo itagharimu kiasi cha  shilingi milioni 10,200,000
 Alilieleza Baraza hilo la  madiwani  kuwa hiyo itakuwa ni awamu ya kwanza ya ununuzi wa mitambo hiyo ya kutengenezea barabara  awamu ya pili itahusu ununuzi wa     Shindilia  model cs 533e  Boza la  maji  na  maloli mawili aina ya Tata
 Diwani wa Kata  ya Kabungu  Selemani Kasonso  akichangia hoja kwenye baraza hilo  alisema mradi huo wa  mitambo ya kutengenezea barabara  utaisadia sana halmashauri hiyo  kujipatia kipato na kutengenezea barabara zake nyingi za vijijini ambazo ni mbavu
 Alisema  mradi huo endapo  hauta simamiwa  vizuri  unaweza kuwa   hauna manufaa yoyote kwenye halmashauri na  matokeo yake  unaweza kuisababishia  hasara Halmashauri hiyo
 Nae  Diwani wa viti maalumu Tiodela Kisesa  alieleza  kuwa mitambo hiyo itakapo nunuliwa ni  vizuri ikatumiwa  kwa ajiri ya Halmashauri na sio  kwa ajiri ya kuwanufaisha watu wachache kwa manufaa yao binafsi
Diwani wa Kata ya Mpanda ndogo Hamad Mapengo  aliliomba Baraza hilo kuwahakikisha mchako huo wa ununuzi wa mitambo uwe ni wawazi kwa kile alichohofia  kuwa kunaweza kukawa na udanganyika katika ununuzi badala ya kununua mitambo mipya ikanunuliwa mitambo ya zamani
Kwaupande wake Mbunge wa jimbo  la Mpanda vijijini Moshi Kakoso  alilieleza baraza hilo  kuwa  mradi  huo wa mitambo ya kutengenezea barabara madiwani wasiuone kuwa ni mdogo
 Alisema  Halmashauri nyingi hapa  nchini hazina mitambo kama hiyo hivyo Halmashauri kununua mitambo hiyo itakuwa imewajengea heshima kubwa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa