Home » » WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI YA MIZENGO PINDA WAFANYA FUJO BALAA, WAVUNJA MAJENGO YA SHULE NA NYUMBA ZA WALIMU

WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI YA MIZENGO PINDA WAFANYA FUJO BALAA, WAVUNJA MAJENGO YA SHULE NA NYUMBA ZA WALIMU

Na Walter Mguluchuma,
Mpanda.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda  kata ya Kibaoni  Wilayani Mlele wamemshambulia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo na mwalimu wa taaluma na kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu hao  baada ya kuwatuhumu walimu hao kuwa ni washirikina.
Kaimu kamanda wa poli wa mkoa wa katavi Joseph Myovela alisema tukio hilo limetokea hapo juzi majira ya saa 2:30 usiku
Alisema chanzo cha tukio hilo kilitokana na mwanafunzi mmoja hapo juzi majira ya saa saba mchana kushikwa na ugonjwa wa mapepo uliomfanya aanguke chini
Aalisema wakati akiwa ameshikwa na mapepo hayo aliwataja ALICO Kamyoge (36) ambaye ni Mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya Mizengo Pinda na mwalimu wa taaluma Bonifasi Nsalamba (35) kuwa ndio wamemroga ugonjwa huu wa mapepo
Myovela alisema ndipo ilipotimia muda huo wa saa mbili wanafunzi hao walipojikusanya na kuandamana hadi kwenye jengo la utawala na kuanza kulishambulia kwa mawe na matofali na kuweza kuvunja mlango na dirisha la jingo hilo.
Alieleza baada ya kufanya uharibifu kwenye jengo la utawala walielekea kwenye ofisi ya mwalimu wa taaluma ambapo waliharibu mtandao wa mawasiliano kwenye Computer.
Wanafunzi hao ambao muda wote walikuwa na hasira walielekea nyumbani kwa mkuu wa shule huku wakiwa na matofali na mawe walipofika na kumkosa mkuu wa shule aliyekuwa amekwenda kwenye matembezi ya jioni walianza kushambulia nyumba yake kwa mawe na tofali na kuharibu mlango na madirisha.
Kaimu kamanda Myovela alisema kisha kundi hilo lilielekea nyumbani kwa mwalimu wao wa taaluma Bonifasi Nsalamba ambapo walimkuta akiwa anajiandaa kuingia ndani ya nyumba yake akitokea matembezini.
Alieleza ndipo walipoanza kumshambulia kwa mawe katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku wakimzomea kuwa mchawi huyo mshirikina walizomea hivyo.
Alisema katika shambulio hilo wanafunzi walimjeruhi mwalimu Bonifasi na kumsababishia majeraha katika mwili wake na aliweza kutibiwa katika zahanati ya kibaoni na kuruhusiwa na hari yake inaendelea vizuri.
Jeshi la polisi mkoa wa katai limetoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine  za mkoa huo waachane na kuamini imani za ushirikina na polisi inaendelea na uchunguzi  wa tukio hilo ili kuwabaini waliohusika na waweze kuchukuliwa hatua.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa