Home » » WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YARIDHISHWA NA VYUO BINAFSI VYA UALIMU

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YARIDHISHWA NA VYUO BINAFSI VYA UALIMU

Na Walter Mguluchuma, 
Mpanda.

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini imetakiwa kupitia upya sera yake juu ya uendeshaji wa vyuo binafsi vinavyotoa mafunzo ya ualimu nchini ili kuviwezesha vyuo hivyo kutoa taaluma stahili ya ualimu kwa ajili ya kuboresha stadi na elimu kwa wanachuo wanaohitimu kupitia vyuo hivyo.

mkuu wa chuo cha ualimu cha St. Aggrey Chanji kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Danford Kabuje alisema hayo jana wakati akisoma  risala kwa mgeni rasmi kaimu mkuu wa mkoa wa rukwa, moshi chang’a, wakati wa mahafali ya kwanza kwa wahitimu wa stashahada na ya pili kwa wahitimu wa daraja la iii a.

alisema kuwa licha vyuo binafsi kuwa  ni sehemu ya wadau wa elimu hapa nchini lakini mfumo uliopo hivi sasa wa kutovishirikisha vyuo binafsi  katika misaada ya hali na mali inayotolewa na serikali kwa vyuo vya umma inavinyima vyuo hivi fursa ya kuinua sekta ya elimu nchini.

Naye,  Mkuu wa wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a alisisitiza umuhimu wa walimu kuzingatia miiko na maadili ya taaluma yao,  sambamba na kuepuka vitendo vinavyosababisha kutokea kwa momonyoko wa maadili katika jamii hivyo kufanya taaluma ya ualimu kudharaulika.

Chang’a alisema kuwa baadhi ya walimu kutofuata maadili na kuzingatia miiko ya kazi yao ndio kiini mmomonyoko wa madilii kwenye kwani wamekuwa na tabia chafu ambazo haziendani na kazi yao hali inayopelekea watoto kuiga tabia hizo pindi wapopelekwa shule kwa lengo kupata elimu.

Aliongeza kuwa hiyo ni changamoto kwa walimu kuhakikisha wanasimamia maadili na miiko ya kazi yao hali itayosaidia kukuza maadili ya watoto nyakati watakazo kuwa shuleni.

Mmoja wa wanachuo wanaohitimu elimu hiyo, Boniventure Ngassa ameitaka Serikali kuhakikisha inaiweka mazingira mazuri ya kujenga miundombinu yatakayowavutia wanafunzi shule za ekondari kuanzia ngazi ya chini kupenda kusoma masomo  sayansi ili taifa lisikose wataalamu wanaotokana na masomo hayo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa