Home » » JELA MIAKA SITA KWA WIZI WA MILIONI 34

JELA MIAKA SITA KWA WIZI WA MILIONI 34

Na Waler Mguluchuma
Mpanda
Mahakama ya hakimu mkazi  ya Wilaya  ya Mpanda  Mkoa  wa Katavi  imemuhukumu Yona   Enerest (42)  mkazi wa   Kijiji  cha Majimoto  Tarafa ya Mpimbwe  kifungo   cha  miaka  sita  jela  kwa  kosa la wizi  wa kuamiwa.
Hukumu   hiyo ilitolewa  hapo juzi na  Hakimu  mkazi    mfawidhi   wa  mahakama ya Wilaya   ya  Mpanda Chiganga  Tengwa  baada ya   kuridhika na  ushahidi ulio tolewa mahakamani  hapo
Awali  mwendesha  mashitaka   Inspekita  msaidizi   Ally Mbwijo  aliiambia  mahakama  kuwa  mshitakiwa  Yona  hapo    April mwaka jana alichukua   jumla  ya    shilingi  milioni 34 kwa  Ismail Salehe  mkazi wa  Mkoa  wa Morogoro  kwa lengo  la kumnunulia  mpunga
Alisema  baada  ya kuwa  amepewa  pesa  hizo  hakununua  mpunga    kama walivyo  kuwa  wamekubaliana  na kila alipo  kuwa akiagizwa   amtumie   mpunga wake  alikuwa akimdanganya  kuwa  eneo  ulipo  mpunga    kunatatizo    la  usafiri  na magari  hayafiki huko
Mwendesha mashitaka Ally Mbwijo  alieleza   kuwa   Isumail  alipo ona  mpunga wake   amechelewa  kuupata  aliamua  kuufuatilia kwa  mshitakiwa  na alipo  ambiwa   amkabidhi  mpunga wake  hata hivyo  mshitakiwa  hakuweza  kufanya hivyo
Hakimu   mkazi   Chiganga  baada ya kusikiliza  uhahidi   ulio tolewa  mahakamani  hapo  alieleza  kuwa mshitakiwa  amepatikana na hatia  ya kujipatia pesa  kwa njia ya udanganyifu  hinyo mshitakiwa  Yona Ernest  amehukumiwa kifungo  cha miaka sita jela na mali zake  ziuzwe  ili  kulipia deni  la milioni 34
Wakati  huo  mahakama hiyo ya Hakimu  mkazi  imemuhukumu  Lubeni  Obedi   (25)  mkazi  wa kijiji  cha  Ilunde  Wilaya  ya Mlele kifungo   cha  miaka mitano  jela  kwa kosa la kuvunja  na kuiba  bidhaa mbalimbali  za dukani
Hukumu  hiyo ilitolewa  na Hakimu  mkazi   mfawidhi   wa mahama ya wilaya  ya Mpanda Chiganga Tengwa.
Mshitakiwa alidaiwa kiiba mafuta  ya taa lita 40,  viberiti  vya chuma  50,  bunda    20 za  sigara  pamoja na pesa tasilimu  shilingi 15,000 mshitakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo hapo oktoba 15 mwaka jana

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa