Na Walter
Mguluchuma
Mpanda jeshi la
Polisi Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi limekamata katoni 16
za pombe kari aina ya Vodka zilizo
ingizwa kutoka Nchi jirani ya Burundi bila kulipiwa
ushuru
Kamanda wa polisi wa
Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema pombe hizo ziiizo kuwa
zimetokea Nchi jirani ya Burundi zilikamatwa hapo Aprili 13
mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika maeneo ya
soko la Bzogwe
Alimtaja aliye kamatwa
na pombe hizo kuwa ni Hadija Hussein
(40) mkazi wa Mkoa wa kigoma aliye kamatwa na
pombe hizo muda mfupi baada ya kuingia mjini Mpanda akiwa anatokea Mkoani Kigoma
kwa kutumia basi la kampuni ya Adventure
Alisema Hadija alikamatwa
kufuatia taarifa zilizo lifikia jeshi la
polisi kutoka kwa raia wema kuwa anajihusisha na
uwingizaji wa pombe karl kutoka Nchi jirani bila
kulipia ushuru.
Kamanda Kidavashari alieleza baada ya
jeshi la polisi kupata taarifa
hizo lilianza uchunguzi wa kumfuatilia mfanya
biashara huyo wa kutokea Kigoma
Ndipo ilipo fikia siku hiyo polisi waliokuwa wakiongozwa na Operation
ofisa wa jeshi hilo wa Mkoa wa
Katavi Timithi Nyika walipo fanikiwa kumkamta mtuhumiwa
Hadija akiwa na katoni 16 za pombe kari aina
ya Vodka
Kidavashari alisema mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa
mahamani mara baada ya upelelezi kuwa umekamilika mapema
wiki lijalo
Jeshi la
polisi Mkoa wa Katavi limetowa wito kwa wananchi kutoa
ushirikiano kwa polisi katika kuwafichua wafanya
biashara wanao igiza bidhaa bila kulipia ushuru na
kuisababishia Serikali kukosa mapato
Baadhi ya wafanya
biashara wamekuwa wakikwepa kulipia ushuru wa
bidhaa zinazo toka katika Nchi za Burundi na
DRC kwa kupitia mwambao mwa ziwa Tanganika
0 comments:
Post a Comment