Na Walter
Mguluchuma
Mpanda
Mahakama ya Hakimu mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imehukumu Sindembala Msagi (26) mkazi wa kijiji cha Bulembo ya wakimbizi ya Katumba wilaya ya Mlele kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka kikongwe mwenye umri wa miaka( 90)
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa baada ya kulidhika na ushahidi ulio tolewa mahamani hapo na pande wa mashitaka na utetezi
Awali katika kesi hii mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspekita msaidizi Ally Mbwijo alidai mahamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa
hilo Desemba 23 mwaka jana nyumbani kwa kikongwe huyo aliye kuwa ana tatizo la ugonjwa wa kupoza mguu na mkono wa kushoto
Mshitakiwa Sindembala alidaiwa siku hiyo majira ya saa tano usiku alikwenda nyumbani kwa mama huyo aliye kuwa akiishi peke yake na kubomoa mlango wa nyumba ya mama huyo na kisha kuingia ndani
Mwandesha mashitaka alieleza mshitakiwa baada ya kuingia ndani alimshika kwa nguvu kikongwe huyo na kuanza kumbaka licha ya
mama huyo kupiga mayowe hakuweza kupata msaada kwa majirani kutokana nyumba ya mama huyo kuwa mbali na majirani wenzake
Kikongwe huyo alijaribu kumsihi mshitakiwa afimfanyie kitendo hicho kutokana na umri wa mama huyo kuwa mkubwa na tendo hilo alisha liacha miaka mingi iliyo pita
Alisema mahamani hapo mshitakiwa Sindembala aliombwa na mama huyo amwache kumbaka na akawatafute wanawake wanao lingana nae lakini mshitakiwa aliendelea kumbaka kikongwe bila kujari uzee wake
Mwandesha mashitaka Ally Mbwijo aliendelea kueleza mshitakiwa baada ya kumbaka mama huyo kwa muda mrefu alijikuta amechoka na kupatwa na usingizi ulio mfanya alale ndani ya chumba cha kikongwe
Ilipo timia muda wa saa 12 alfajiri mama huyo alifungua dirisha na kumwona mtu mmoja akipita aitwaye
Abushola Elly jirani na nyumba yake ndipo alipo mwita kwa ishara ya vidole na mtu huyo aliweza kuitikia wito na mama huyo alimwoleza kuwa amebakwa na aliye mbaka bado yumo ndani amesinzia
Mtu huyo ambae alikuwa shahidi katika kesi hii aliingia ndani na kumkuta mshitakiwa akiwa bado amelela na baada ya kuwa
amemtambua aliogopa
kumkamata akiwa peke yake kutokana na tabia aliyo kuwa nayo mshitakiwa Sindembula ya ukorofi na ugomvi hari ilyo mfanya akimbie kwende kuwaita majirani
Mwendesha mashitaka alieleza majirani walipo fika katika eneo hilo walimkuta mshitakiwa akiwa ameondoka ndipo wananchi wa kijiji hicho wakishirikiana na polisi wa kituo cha Kanoge walipo weza kufanikiwa kumkamata
mshitakiwa kabla ya kufika nyumbani kwake
Katika utetezi wake mshitakiwa aliomba mahakama imwachie huru kutokana na ushahidi ulio tolewa dhidi yake kuwa ulikuwa wa uongo
Hakimu mkazi mfawidhi Chiganga alisema mahamani hapo kuwa katika kesi hiyo ameridhika na mwenendo mzima wa kesi
kwa ushahidi wa pande
hizo mbili za
mashitaka ambao ulikuwa na mashahidi wanne na mshitakiwa aliye jitetea mwenyewe
Alisema kutokana na ushahidi huo mshitakiwa amepatikana na hatia ya kuvunja sheria ya kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu cha marekebisho ya mwaka 2002
kutokana kosa hilo mahama imemuhukumu mshitakiwa Sindembali Msagi kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 30 kwa kitendo
chake cha kumbaka kikongwe huyo
Mahakama wakati wa kuisikiliza kesi hiyo illazimika huhamia nyumbani kwa mama huyo kusikilizia kesi hii kutokana na kikongwe huyo kutokuwa na hari nzuri ya
kiafya toka alipo
fanyiwa kitendo hicho
0 comments:
Post a Comment