Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Watu wawili wakazi wa kijiji cha Matandalani wilaya ya mlele Mkoa wa Katavi wameuwawa na wananchi baada ya kukili kuiba mbuzi dume wa mwanakijiji mwenzao
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwataja walio uwawa kuwa ni Alex Kazimoto (28) Tonora
Luchagula (30) wote
wakazi wa
kijiji cha
Matandalani
Alisema tukio hili lilitokea Aprili 14 mwaka huu majira ya saa saba mchana ambapo chanzo cha vifo vya watu hao vilitokana na wizi wa mbuzi walioiba hapo Aprili 10 nyumbani kwa Jacob Sekela
Jacob baada ya kugundua mbuzi wake dume ameibiwa alikwenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji hicho Malcus
Wimbi ambae nae aliwapa jukumu askari mgambo wa kijiji hicho kumtafuta mbuzi huyo aliye ibiwa
Kamanda Kidavashari alieleza ndipo askari mgambo walimkamata Tonora Luchagula na walipo muhoji alikiri kuiba mbuzi huyo akiwa na marehemu Alex Kazimoto na ndipo mgambo hao walipo wachukua watuhumiwa na kuwapeleka nyumbani kwa mwenyekiti
Ndipo ilipo timia saa 2 usiku kundi la watu lililo jiita Mwano lilifika nyumbani kwa mwenyekiti na kumwamuru mwenyekiti
awape watuhumiwa hao baada ya mwenyekiti kuwakatalia walianza kumshambulia na kufanikiwa kuwatoa watuhumiwa na kuondoka nao na walimuonya mwenyekiti
asiwafuate vinginevyo watamuuwa
Kamanda alisema kundi hilo lilikwenda na watuhumiwa hadi
nyumbani kwa Donard Sorera ambae ndie anadaiwa kuwa ndiye aliye watuma kwenda kuiba mbuzi huoyo walipo mkosa ndipo walipoanza kuwashambulia wahuhumiwa kwa kutumia silaha za jadi hadi kufa
Katika tukio hilo watu wawili Deus Zegula na Malcus Wimbi wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na mauwaji ya watu hao kwa ajiri ya maojiano
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limetoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mikononi na badala yake watowe ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutowa taarifa ambazo zitaweza kuwabaini watuhumiwa wanao husika na matukio kama haya ili waweze kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dora na sheria iweze kuchukua mkondo wake
0 comments:
Post a Comment