Na
Walter Mguluchuam
Sumbawanga.
JESHI la polisi
Mkoani Rukwa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuzuia askari
magereza kufanya kazi ya kumkamata Mfungwa aliyetoroka katika gereza
za mahabusu la Sumbawanga ,aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 15 jela
baada ya kupatikana na hatia ya unganganyi wa kutumia silaha.
Aidha katika tukio
hilo askari wa magereza walimjeruhi kwa risasi kijana Isiaka Andrea
mwenye(17) ambaye ni mdogo wa mfungwa aitwae Nizal Paschal
alitoroka kifungo chake mwaka mmoja uliopita baada ya kutumikia
kifungo cha mwaka mmoja gerezani .
Akizungumza na vyombo
vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda amesema
kuwa tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika kijiji cha
Isesa kilichopo katika manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, na
kuwataja vijana hao wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni Mosea
Andrea(19),Pamoja na Nduguye aitwae Isiaka Andrea(17) ambaye
amelazwa ward namba tatu ya hospitali ya mkoa wa rukwa
akitibiwa jeraha la risasi lililopo katika mguu wake wa kulia
Akifafanua juu ya
tukio hilo kamanda Mwaruanda amesema kuwa inadaiwa kuwa askari hao
waliizingira nyumba hiyo mara baada ya kupata taarifa za siri toka kwa raia
wema zilizoeleza kuwa mfungwa aliyetoroka gerezani mwaka mmoja uliopota amerudi
na kuungana na familia yake na ndipo siku ya tukio majira ya jioni askari hao
wa magereza walifika katika nyumba hiyo kwa lengo la kumkamata kijana huyo ili
sheria iweze kuchukua mkono wake.
Alisema kuwa hata
hivyo mara baada ya kufika katika nyumba hiyo ndipo vijana hao pamoja na
nduguyao ambaye alifanikiwa kutoroka mara baada yaa kugundua kuwa
waliopo nje ya nyumba yao ni askari walitoka wakiwa na silaha za jadi mikononi
mwao kwa lengo la kutaka kuwajeruhi askari hao na kwa bahati nzuri askari mmoja
alifyatua risasi iliyomjeruhi kijana huyo mguuni.
Kamanda Mwaruanda
alisema kuwa mara baada ya vijana hao kuona askari hao wametumia silaha hiyo ndipo
walipotupa silaha zao za jadi ambazo ni mapanga mishare na marungu jambo
lililofanikisha askari hao kuwakamata huku mfungwa aliyetoroka gerezani
akifanikiwa kuwakacha askari hao
Kwa upande wake baba
mzazi wa mfungwa huyo aliyetoroka na kusababisha kizazaa kwa familia yake Bw
Paschal Andrea amesema kuwa majira ya saa sita usiku
nyumba yake ilivamiwa na askari magereza saba ambao kwa usiku huo hakuweza
kutambua kuwa ni askari kutokanaa na kiza kinene kutanda ,na kisha askari
hao bila ya kufuata taratibu na kufyatua risasi iliyomjeruhi kijana
wake,
Alisema kuwa mara
baada ya kijana wake kujeruhiwa alianza kupiga kelele za kuomba msaada ndipo
mzee huyo ambaye alikuwa amelala na kuamshwa kwa kelele za risasi
alipotoka na kisha nae kuambulia kipigo toka kwa wajela hao ambao
alifanikiwa kuwatoroka muda mfupi baadaye.
Naye Mwenyekiti wa
kijiji hicho cha Isesa Bw Revocatus Kasuku licha ya
kulaani kitendo hicho cha kijana huyo kujeruhiwa kwa risasi amesema
kuwa kwa kipndi kirefu sasa watumishi wa jeshi la polisi
wamekuwa wakifika katika kijiji hicho na kuendelea na oparesheni mbalimbali
bila ya kuwashirikisha w viongozi wa maeneo hayo.
Bw Kasuku amesme kuwa
kutokana na vitendo hivyo kuendelea kwa muda mrefu sasa amekwisha peleka barua
ya malalamiko kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya
sumbawanga ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo na anasubiri utekelezaji wake.
0 comments:
Post a Comment