Home » » AUAWA BAADA YA KWENDA KUOMBA GAZETI LA KUVUTIA SIGARA

AUAWA BAADA YA KWENDA KUOMBA GAZETI LA KUVUTIA SIGARA

Na  Walter Mguluchuma
Mpanda
Jeshi  la polisi  mkoa   wa Katavi  linamshikilia  Albert  Ades (25) mkazi   wa Katandala  Sumbawanga   kwa  tuhuma   za  kumuuwa Yassin Lupinda  (22) kwa kumchoma   na kitu  chenye  ncha  kali  kufuatia  marehemu  kumwomba gazeti  la kuvutia sigara
Kamanda  wa poilisi  wa  Mkoa wa Katavi Dhahiri kIdavashari  alisema tukio hilo  lilitokea Aprili 12 majira ya saa 6 usiku  katika kambi ya uvuvi  wa samaki  ya  mtakuja  Tarafa ya Mpimmbwe Wilayani Mlele Mkoa wa katavi
Alisema  siku  hiyo  ya tukio  marehemu  alikwenda  kuomba  gazeti  la kuvutia  sigara  kwenye kambi   jirani   ya uvuvi  aliyo  kuwa akiishi  mtuhumiwa 
Kidavashari alieleza  baada  ya marehemu  kufika   kwa mtuhumiwa  na  na kueleza  shida yake  ya kuomba  gazeti  la kuvutia  sigara mtuhumiwa  alimweleza  marehemu  kuwa  hayuko  tayari  kumpatia  gazeti  la  kuvutia zigara
Marehemu Yassin aliendelea kumsihi  mtuhumiwa   amsaidie kipande  hata  kidogo  tuu  cha gazeti  kutokana  na kiu  kubwa aliyo kuwa aiisikia  ya  ya kuvuta  sigara
Hata hivyo mtuhumiwa  aliona  kama  imekuwa  kwake   ni kero   kwa marehemu  kuendelea  kumwomba  kipande  cha gazeti   la kuvutia  sigara
Kamanda  Kidavashari  alieleza  ndipo  marehemu  alipo  taka kuchukua  gazeti  kwa nguvu  kitendo   ambacho  hakikumridhisha  mtuhumiwa  Albert
Ndipo  ulipo  tokea  ugomvi  na  mtuhumiwa  alipo   mchoma   marehemu  kwa kitu  chenye  ncha  kali   sehemu  ya  kifua  na kumfanya apige  mayowe  ya kuomba msaada
Majirani  wa kambi   za  wavuvi   walifika  kwenye  eneo  hilo  na  walimkuta  Yassin akiwa  amegalagala  chini  huku  akiwa  amelala kwenye  dimbwi la damu  na walipo jaribu  kumwinua  waligundua  ameisha  kufa  na  wavuvi  hao walifanikiwa  kumkamata  mtuhumiwa muda huo huo
Kamanda  Kidavashari  alisema  mtuhumiwa  anatarajiwa  kufikishwa  mahamani  kujibu  shitaka  la  huhuma   za mauwaji  mara baada  ya    upelelezi utakapo  kamilika

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa