Home » » CHUO KIKUU CHA KILIMO KUJENGWA KATAVI

CHUO KIKUU CHA KILIMO KUJENGWA KATAVI

Zaidi  ya Shilingi Bilioni 4.5 zinatarajiwa kutumika kwaajili ya mchakato wa awali wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Katavi , kinachotarajiwa kujengwa mjini Mpanda.

Akizungumzia ujenzi huo Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Mpanda Bw. Joseph Sebastian Mchina amesema kiasi hicho cha fedha kimepatikana ikiwa ni mkopo kutoka benki ya African Trade Insurance Agency (TIA).

Bw. Mchina amesema fedha hizo zitatumika kwaajili ya kulipa fidia ya eneo la ardhi  lenye ukubwa wa hekari mia tano, ambazo zinatarajiwa kujengwa chuo hicho sanjari na gharama za andiko la mradi wa chuo hicho.

Mkurugezni huyo amesema chuo hicho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Kazima nje kidogo ya mji wa Mpanda ambapo katika matumizi ya fedha za awali pia mtaala wa chuo hicho utaandaliwa.

Amesema chuo hicho licha kujengwa mjini Mpanda kinatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa mikoa jirani ya Rukwa na  Kigoma ambapo katika hatua za ujenzi wa majengo yake jumla ya Shilingi Bilioni 650 zinatarajiwa kutumika ikiwa ni ruzuku kwa asilimia themanini  na mkopo kutoka kwa Wafadhili kutoka nje ya nchi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa