Home » » KIZIMBANI KWA KUMBAKA MTOTO WA MWAKA MMOJA NA NUSU

KIZIMBANI KWA KUMBAKA MTOTO WA MWAKA MMOJA NA NUSU

Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Mkazi   wa  Kijiji   cha Karema    Wilaya Mpanda Mkoa wa Katavi Jonas  Ndegela ( 63) amefikishwa  katika mahakama ya Hakimu mkazi   ya wilaya ya Mpanda  kwa tuhuma za  kumbaka  mtoto wa  dada  yake  mwenye umri  wa  mwaka mmoja  na  nusu Mwendesha  mashika  wa  jeshi  la polisi  wa jeshi la  polisi  Ally Mwijo  aliiambia  mahakama mbele ya hakimu  mkazi  mfawidhi   wa mahama   hiyo  Chiganga Tengwa   kuwa  mshitakiwa  alitenda  kosa  hilo   Aprili  6 mwaka huu majira ya saa 5 asubuh
Mshitakiwa  anadaiwa   kuwa  siku  moja  kabla ya kufanya tukio hili  alikuwa ametokea  kijiji  cha   Karema  kwa lengo  la  kumsalimia dada  yake  ambae  ni mama  wa mtoto  huyo aliye mbaka  walio kuwa wakiishi  katika kijiji  cha   Mnyamasi  Kata ya Mpanda ndogo
Mwendesha mashitaka  alieleza kuwa  siku hiyo  baada ya  kuwa  amefika  kijijini   kwa dada yake  aliondoka  na  jirani  ya    mwenyeji wake  na kwenda  kwenye  kilabu   cha pombe  za  kienyeji  ambapo  alikunywa pombe  na kuzidiwa  na kisha  kulala kwenye  kilabu   hiyo  ya pombe  za kienyeji
Mshitakiwa Jonas  baada ya kuamka  alielekea  nyumbani kwa dada yake  aliko  kuwa  amefikia  ambapo alipo  fika   hakumkuta  dada yake  ila mlango  wa nyumba  yake  ulukuwa uko  wazi
Hari hiyo  ilimfanya mshitakiwa aingie  moja kwa moja  ndani  na ndipo alipo ingia ndani  alimwona  mtoto huyo wa dada yake  akiwa amelala  peke yake
Mshitakiwa  alimwinua  mtoto  huyo bila huruma  alipo kuwa amelala  na  kisha  alivua   nguo  zake  na  kumweke  juu ya  kifuu chake  na kisha  alanza  kumfanyia bila huruma  kitendo   cha  kumbaka  huku  mtoto  huyo  akipiga  kelele
Mwendesha mashitaka aliendelea kuiambia mahakama  kaka   wawili wa mtoto huyo  walio kuwa wameachiwa wamuangalie mdogo wao na mama yao aliye  kuwa amekwenda kisimani kuteka maji  waliposikia mtoto analia  waliingia ndani  aliko kuwa amelala  mtoto na walishitushwa  kuona mjomba wao  akimfanyia   unyama mdogo wao   na kuwafanya watoke nje  haraka   na kwenda kuwaharifu majirani
Majirani walifika  katika eneo hilo  na  kumkuta  mshitakiwa   akiwa  anajiandaa  kuvaa nguo  zake   alizo kuwa amezivua   huku  mtoto huyo akiwa  akilia kutokana na maumivu   makali aliyo  kuwa nayo
Mshitakiwa baada ya kuulizwa na majirani  kwani amemfanyia  unyama   mtoto wa dada yake  aliwaeleza   kuwa ni kutokana na pombe  alizo  kuwa  amekunywa  usiku   kucha
Mshitakiwa  alikana shitaka na  hakimu   mkazi  mfawidhi  Chiganga  aliharisha   kesi hiyo    hadi   hapo  Aprili  25  kesi  hiyo  itakapo  tajwa   tena  na  na mshitakiwa   amepelekwa  rumande baada  ya  kunyimwa mdhamana

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa