MKAZI wa kijiji cha Majimoto wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi ,Justine Albert (24) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya
Mpanda akikabiliwa na makosa matatu ya mauaji .
Justine alifikishwa jana (Ijumaa) mbele ya Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama hiyo , Kiganga
Tegwa akishitakiwa kuwaua watoto wake wawili ambao ni Justine (6) na Eliza Justine (4) na mama yao Jacqueline
Luvika (21),.
Hata hivyo
Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusilikiza shauri hilo ambalo litasikilizwa katika Mahakama Kuu .
Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi Ally Bwijo aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda ukatili huo Aprili 06, mwaka huu saa 11:30 alfajiri ambapo aliwaua watoto wake hao wawili kisha miili yao na mama yao akiwa hai wakatumbukizwa katika kisima cha maji kijijini Majimoto .
Ilidaiwa pia kuwa mama huyo aliyetumbukizwa hai katika kisima cha maji pamoja na miili ya watoto wake hao wawili kijijini humo
alifariki dunia Aprili 07, mwaka huu
katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda alikohamishiwa kwa matibabu .
Ndipo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo , Tengwa alipolazimika kuahirisha kesi hiyo Aprili 25 mwaka huu ambapo imepangwa kutajwa tena kwa kuwa upande wa mashtaka bado hawajakamilisha upepelezi wake ila mshtakiwa ataamriwa kurejeshwa rumande.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa kutoka kijijini Majimto pia zimethibitishwa
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari kulipopambazuka siku hiyo ya tukio , Aprili 06 ,mwaka huu baadhi ya wakazi wa kijiji hicho cha Majimoto , walio kuwa wakienda kwenye shughuli zao , waliuona mwili wa mtoto ukiwa umetelekezwa kando ya njia na kumtambua kuwa ni Maria mwenye umri wa miezi minne ambaye ni kitinda
mimba katika familia hiyo .
Inadaiwa wakazi hao waliamua kwenda nyumbani kwa
mtuhumiwa, kumpatia taarifa hiyo huku wakiuliza mama wa mtoto aliko. Kamanda
Kidavashari alidai mtuhumiwa aliwaeleza wakazi hao kuwa mama wa mtoto huyo,
alikuwa ametoroka kwenda kusikofahamika na watoto wote ndipo wakazi hao wapomtilia shaka mtuhumiwa, wakaamua kutoa
taarifa kituo cha Polisi kijijini hapo, ambao walifika ulipo mwili wa mtoto
Maria wakidhani kuwa
ni mfu .
Wakati wakiwa katika
eneo la tukio, Kamanda Kidavashari alidai walibaini alama za mburuzo ardhini,
wakaanza kuifuatilia na zikawafikisha kisimani. Walipofungua mfuniko wa kisima
hicho, walishtuka kuona miili wa watu watatu, ikielea kwenye maji kisimani
humo.
Askari Polisi kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji
hicho, waliopoa miili yote, lakini watoto hao wawili tayari walikuwa
wamefariki, huku mama yao akiwa amekunywa maji mengi na kupoteza fahamu na kukimbizwa katika Kituo cha Afya kijijini Mamba kwa matibabu lakini alifariki siku iliyofuata jioni katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda akikohamishiwa kwa matibabu ..
0 comments:
Post a Comment