Home » » MAPOKEZI YA MWILI WA ASKOFU PASCAL KIKOTI WA JIMBO LA MPANDA‏

MAPOKEZI YA MWILI WA ASKOFU PASCAL KIKOTI WA JIMBO LA MPANDA‏


 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda kabla ya kuupokea mwili wa marehemu Askofu wa Kanisa Katoriki Jimbo la Mpanda aliyefariki dunia Jumanne ya Wiki hii kutokana na shinikizo la damu katika Hospitari ya Rufaa ya Bugando Mkoani Mwanza Askofu Kikoti anatarajiwa kuzikwa kesho ndani ya Kanisa kuu la Mtakatifu Emakurata la Jimbo la Mpanda.
Ndege iliyouleta mwili wa marehemu Pascali Kikoti baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda ikitokea Mjini Mwanza hapo jana.
Mapadri wa Kanisa Katoriki wakiwa wameubeba mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoriki Jimbo la Mpanda Pascal Kikoti mara baada ya kutelemshwa kwenye ndege kutokea Mwanza
Waumini watatu wa kanisa Katoriki Jimbo la Mpanda wakiwa wamelazwa kwenye wodi maalum iliyokuwa imeandaliwa kwenye ukumbi wa kanisa  Katoriki wakiwa wamepoteza fahamu mara baada ya mwili wa Askofu wa Jimbo la Mpanda Pascal Kikoti ulipowasiri kwenye Kanisa kuu la Kiaskofu la Jimbo la Mpanda.

Maelfu ya wakazi wa Mji wa Mpanda waliojitokeza kuupokea mwili wa marehemu Askofu wa Jimbo la Mpanda Pascal Kikoti wakitokea katika uwanja wa ndege wakielekea kanisa kuu la jimbo la Mpanda  Picha na Walter Mguluchuma katavi.



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa