Na Walter Mguluchuma
Mpanda – Katavi yetu blog
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda jana aliongoza maelfu ya wakazi wa Mji wa Mpanda kuupokea mwili wa Askofu wa Kanisa la Katoriki Jimbo la mpanda aliye fariki Jumanne wiki hii katika Hospitali Bugando Mwanza.
Mwili wa Askofu Pascal Kikoti uliwasiri katika uwanja wa ndege wa mpanda mnamo majira ya saa 10:40 jioni na kufanya eneo hilo la uwanja wa ndege kuwa na simanzi kubwa ya wananchi ambao walikuwa hapo toka saa nane mchana wakisubiria kuwasiri kwa mwili wa Askofu Kikoti.
Mbali ya Waziri Mkuu, Miongoni mwa viongozi waliojitokeza kupokea mwili wa Askofu Kikoti ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Rajab Rutengwa, Katibu tawala wa Mkoa huo Injinia Emmanuel Kelobelo na wakuu wa Wilaya za Mpanda na Mlele.
Pia walikuwepo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Paulo Buzoka na Askofu wa Jimbo la Sumbawanga Damiano kiaruzi na Askofu wa Jimbo la Kahama Rudovic Minole pamoja na watawa wa kike na wa kiume.
Msafara wa kuupeleka mwili wa marehemu Kikoti kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda ulichukua zaidi ya saa 1:30 hadi kufika kwenye Kanisa la Parokia kuu ya Mpanda kutokana na umati mkubwa ambao haujawahi kutoka Mjini Mpanda.
Baada ya mwili wa Askofu Kikoti kuwasili kwenye kanisa kuu la Jimbo la Mpanda kulifanya badhi ya waumini kulia hadi kuzirai na kulazwa katika wodi ya ukumbi wa kanisa hilo kwa ajili ya kupatiwa matibabu uliokuwa umeandaliwa toka awali.
Kisha ilifanyika Ibada Misa ya kumuombea marehemu Askofu Pascal Kikoti ambayo pia ilihudhuliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Misa mabayo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora Paulo Buzoka.
Ibada ambayo iliwashirikisha pia maaskofu watano wa majimbo ya Iringa, Sumbawanga, Kahama, Geita na Mwanza.
Kwa upande wake Askofu Mkuu Buzoka katika maubili yake kwenye ibada hiyo elieleza kuwa marehemu Askofu kikoti katika uhai wake alitumia muda mwingi mbali ya kuwaudumia watu kiroho pia ni mtu aliyependa kuleta maendeleo kwa wananchi.
Alisema katika uongozi wake kwa muda mfupi alioongoza jimbo la Mpanda ameweza kufanya mambo mbalimbali kama vile ujenzi wa Kanisa, Zahanati, Sekondari, Seminari pamoja na huduma za maji.
Makamu Askofu wa jimbo la Mpanda Padri Patrick Kasomo alisema Askofu pascal Kikoti anatarajiwa kuzikwa kesho ndani ya kanisa la parokia Kuu la Maria Emakurata baada ya misa hiyo itahudhuriwa na kadinari laurian lugambwa barozi wa Papa Nchini na maaskofu mbalimbali, Mapadri, masista waumini na viongozi wa Serikali na vyama mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment