Home » » WATATU WAKAMATWA NA BUNDUKI TATU ZA KIVITA RISASI 16 MAGAZINE TANO NA MENO YA TEMBO VIPANDE NNE YENYE THAMANI YA TSHS MILIONI 34,050,000

WATATU WAKAMATWA NA BUNDUKI TATU ZA KIVITA RISASI 16 MAGAZINE TANO NA MENO YA TEMBO VIPANDE NNE YENYE THAMANI YA TSHS MILIONI 34,050,000

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
  Kamanda   Damas  Nyanda  akionyesha  gobore     lillokamatwa na  jeshi la  polisi kufuatia  msako waliofanya  jana  huko  katika  Kijiji cha  Ugalla  Wilaya ya  Mpanda .
Kamanda wa  Polisi wa   Mkoa wa  Katavi  Damas  Nyanda   akionyesha  vipande  vya  meno ya   waliokamatwa  nayo watuhumiwa   waliokamatwa wakiwa na  silaha  tatu za  kivita  story imeisha tangulia

Na  Walter  Mguluchuma .
      Katavi .
  Watu  watatu   kati ya  watuhumiwa watano  wanashikiliwa na  jeshi la  Polisi  Mkoa wa  Katavi baada ya kukamatwa  wakiwa   na  silaha     nzito  tatu  na  magazine tano  risasi  16    na  vipande  vinne  vya  mame ya  tembo yenye   thamani ya zaidi ya TSHS 34  baada ya  mabishano ya  risasi  baina yao   na  Askari   Polisi  na  Wahifadi ya  Taifa ya  Katavi  huku watuhumiwa wawili  wakiuawa katika tukio  hilo .
Kwa  mujibu wa  taarifa  iliyotolewa  mbele ya  Wandishi wa  Habari  hapo  jana  na   Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa wa  Katavi  Damas   Nyanda  alisema tukio  hilo   hilo  la kamatwa kwa wathumiwa  hao  watatu na wawili kuuawa  lilitokea  hapo  juzi   majira ya saa  sita  usiku  huko  katika   Kijiji  cha   Kapalamsenga   Wilaya ya  Tanganyika   Mkoani   Katavi .
  Alisema  watuhumiwa  hao walikamatwa  kufuatia   msako   mkali  uliofanywa   kwa muda wa wiki tatu    na  Jeshi la  Polisi na  Askari wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi  ambao walipata taarifa juu ya watu hao kujihusisha  na  maswala ya ujambazi na  ujangili  ndani ya  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi .
Baada  ya      kuwa  wamepata  taarifa  hizo  ndipo  walipo  fanya   msako  huu  uluodumu  kwa  muda wa wiki  tatu  za  kuwasaka  watuhumiwa  hao  ulikuwa ukifanyika  usiku  na   mchana .
Kamanda  nyanda   alieleza  ndipo  hapo  juzi   Askari  hao  walipofanikiwa  kuwakamata watuhimiwa   hao   baada ya  mabishano   makali ya kurushiana  risasi  ambapo  katika  tukio  hilo  watuhumiwa  wawili   kati ya  watano waliweza kuuawa  kwa  kupigwa  risasi .
 Alisema  baada ya    kutiwa  nguvuni   watuhumiwa  hao  walikamatwa  wakiwa  na   bunduki    tatu za  kivita   aina ya  SMG  ,risasi   16,  magazine  tano  na  vipande  vinne    vya  meno  vyenye  uzito wa kilo 6.6  yenye  thamani ya  Tshs  34,050,000.

Pia  watuhumiwa  hao  walikamatwa  wakiwa  na    nyama  ya  pofu  kilo   20   zenye  thamani  ya  Tshs 3,859,000 wakiwa wamehiifadhi  ndani ya  mfuko  wa   sandarusi .
  Kamanda  Nyanda   alisema  watuhumiwa  hao  wanaendelea kushikiliwa  na   jeshi la  polisi  na  wanatarajiwa kufikishwa   Mahakamani   mara   baada ya   upelelezi  utakapo kuwa  umekamilika .
  Kamanda  Nyanda   ametowa  wito  kwa  watu  waheshimu  sheria  na waache  kufanya  uhalifu  kwani  maisha ya uhalifu  ni  mafupi na   amewataka  wananchi  wanapokuwa wameona  viashiria vya uharifu watowe  taarifa  kwenye  vyombo husika .
Mkuu  wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi   Izumbe   Msindai   alisema  ushirikiano wa       Askari wa  Hifadhi ya  Taifa   ya   Katavi na   Polisi  ndio  umefanya watuhumiwa  hao kukamatwa .
Alisema   Hifadhi ya   Katavi  wataendelea  kushirikiana  na   wananchi  wanao  zunguka   hifadhi  hiyo   katika  kukabiliana  na  swala   zima    la   ujangili  wa  wanyama  ndani ya  Hifadhi na  nje ya  Hifadhi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa