Home » » MWANAFUNZI ABAKWA HADI KUFA NA SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZA NYOFOREWA WAKATI AKIWA ANAKWENDA SHULE .

MWANAFUNZI ABAKWA HADI KUFA NA SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZA NYOFOREWA WAKATI AKIWA ANAKWENDA SHULE .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma .
        Katavi .
Mwanafunzi wa    darasa la sita  Shule ya  Msingi  Vikonge Wilaya  ya  Tanganyika  Mkoa wa  Katavi   mwenye umri wa miaka 14  ameuawa  kikatili  baada ya kubakwa na kuchomwa kisu ubavuni  na kisha  kunyofolewa  sehemu za  siri wakati akiwa  anakwenda shuleni na mdogo wake wa liokuwa wakisoma  shule moja .
   Kamanda  wa  polisi wa  Mkoa wa   Damas    Nyanda   alisema  tukio  la   kuuawa kwa  mwanafunzi  huyo wa kike lilitokea  hapo  jana  majira ya saa  moja  na  nusu   Asubuhi umbali wa kilometa  moja na  nusu  kutoka katika    shule ya  Msingi   Vikonge.
 Alisema  siku  hiyo ya  tukio      marehemu  huyo   alitoka  nyumbani kwao   kwa  lengo la  kwenda    shuleni  kama  ambavyo ilivyokuwa   kawaida yake   huku   akiwa  na  mdogo wake wa kiume  mwenye  umri wa miaka 11  mwanafunzi wa   darasa   la  nne  shule ya  Msingi  vikonge  ambae  jina  lake limehifadhiwa .
 Wakati wakiwa  njiani  alitokea  mwendesha  pikipiki  moja    ambae walikuwa  hawamfahamu  na  kusimamisha  pikipikiyake  na  kisha   aliwaambia kuwa  awape   msaada wa      usafiri wa kuwafikisha shuleni  kwao .
Kamanda   Nyanda  alieleza  baada ya  kuambiwa  hivyo  wanafunzi hao walikubali  kupewa  msaada wa pikipiki  hata  hivyo  mara  baada ya  marehemu  kuwa  amepanda pikipiki  hiyo   mwendesha  boda  boda  huyo    alimzuia  mdogo wa marehemu  asipande  kwenye pikipiki  hiyo na kisha  aliiondoa  huku   akiwa na  marehemu na   kumwacha  kaka yake .
 Hari  hiyo  ilimfanya  kaka yake  aamue kuifuata  pikipiki  hiyo kwa  nyuma na  ndipo  wakati  akiwa  njiani  aliona  pikipiki  kama  ile  iliyokuwa imembeba  dada yake ikiwa kwenye kichaka  pembeni ya  barabara  hata  hivyo aliendelea  na  safari yake ya  kwenda  shuleni .
  Kaka  huyo wa marehemu  kutokana  na kuwa na umri  mdogo baada ya kufika  shuleni  hakuweza kumtafuta  dada yake na   badala yake  aliingia  darasani na  kuendelea  na  masomo      kama    kawaida   na   baada ya muda wa  masomo  ilipofikia   majira ya  saa  nane  na  nusu  alianza  safari ya  kurejea  nyumbani pasipo kumtafuta  dada yake.
Kamanda    Nyanda   alieleza   baada ya kuwa  amefika  nyumbani kwao wazazi wake walishituka  kumwona  akiwa  peke  yake  ndipo  walipomuuliza  aliko  mwacha  dada  yake  na   aliwaeleza  mazingira yote  ya jinsi  alivyo  achana  na  dada  yake wakati walipokuwa  njiani  na  jindi alivyoiona   pikipiki  iliyombeba dada yake ilivyokuwa  kwenye kichaka .
   Wazazi wa  marehemu  baada ya  kupata  maelezo  hayo walipatwa na    mashaka   hivyo  walimtaka  mdogo wa marehemu  awapeleke  kwenye  eneo   aliloona  pikipiki  ikiwa     kwenye kichaka .
Alisema  Wazazi wa marehemu waliokuwa wameongozana  na     majirani zao  baada ya kufika  kwenye  eneo  hilo walishitushwa  kuona  majani yakiwa  yakiwa  yamelala  na  ndipo walipoenda  mbele kidogo waliweza kuukuta  mwili wa marehemu  ukiwa  amechomwa  kifu   sehemu ya  ubabu wake wa kulia  na  sehemu za   siri  zikiwa  zimenyoforewa .
  Kamanda wa  polisi Damas  Nyanda  alisema  jeshi la  polisi   Mkoa wa  Katavi  linaendelea na  msako wa  kumtafuta   mtu    au watu waliohusika       na mauwaji hayo ya  kikatili  hadi sasa  hakuna mtu  wla watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo .
Kaimu   mwalimu   Mkuu wa  Shule ya   Vikonge  Mwalimu  Gadinendi   Kaseka  alisema    mpaka   walipomaliza  masomo ya siku  hiyo  hawakuwa na  taarifa juu ya kifo cha mwanafunzi huyo ila walipata taarifa hiyo siku  hiyo  hiyo  majira ya saa kumi na  mbili jioni  baada ya mwili wa marehemu kuwa umepatikana .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa