Home » » WATUMISHI WA MALIASILI KATAVI WATAKIWA KUWA MAKINI NA UTOROSHWAJI WA MAZAO YA MISITU.

WATUMISHI WA MALIASILI KATAVI WATAKIWA KUWA MAKINI NA UTOROSHWAJI WA MAZAO YA MISITU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma.
         Katavi.
 Naibu  Waziri  Waziri  wa  Nchi  wa    ofisi ya  Rais   Tamisemi   George  Kakunda   amewataka  Wa watumishi wa   idara  za  Maliasili   za  Mkoa wa  Kavi  wawe  makini  katika utendaji wao wa kazi  ili kulinda  rasilimali za    mistu  ambazo zimekuwa zikisafirishwa kwa njia ya  panya kwenda katika  Mikoa  mingine  hapa  Nchini .
Kakunda  alitowa kauli  hiyo  hapo  jana wakati  alipokuwa   akizungumza  na  viongozi wa  Serikali wa  Mkoa wa  Katavi katika   ofisi ya  Mkuu wa  Mkoa w a  Katavi  wakati wa   ziara ya  siku  moja   Mkoani  hapa .
  Alisema   Wizara  yake  inayotaarifa  za  utoroshwaji wa  mazao ya  Mistu  kwa  njia za   panya  kutoka  Mkoani  hapa   kwenda   katika    Mikoa   mingine  unaofanywa   na  wafanya  biashara  kwa  njia  ya  za  panya  na  hasa    nyakati za  usiku .
Mazao ya   mistu   yanayotoroshwa  sana   bila  vibali   alitaja  kuwa ni  mbao   ambazo   zimekuwa   zikisafirishwa  kutoka   Katavi  na  kupelekwa  Mwanza  bila kufuata  utaratibu wa  kulipia  ushuru  uliowekwa  na  Serikali .
 Alisema  inawezekana   mazao  hayo ya mistu    yanayosafirishwa kwa njia za  panya  yakawa     nanasafirishwa  na  wafanya  biashara  hao    kwa  kushirikiana  na   watumishi wa  idara za  maliasili   ambao sio  waaminifu .
  Aliwaonya  watumishi wanaofanya  hivyo   kushiriki kuhujumu   rasimali za   mistu kuwa   kwa  wale  watakao  bainika  Serikali itawachukulia  hatua  kali za   kinidhamu  mara  moja  wakakapo kuwa wamebainika  kushiriki  kuhujumu   rasilimali za    za  Nchi  yetu .
 Naibu  Waziri  huyo  alisema  ni   vema  watumishi wa  Halmashauri  wawe  makini  katika  kufanya  kazi  za  kulinda  rasilimali za     mazao ya mistu  kwenye  kila  maeneo yao ili  kuweza  kuwadhibiti  wanao hujumu  rasilimali za   mistu.
Pia  alieleza kuwa  Serikali  inafikilia  kujenga  barabara za  rami  kwenye  kila   Halmashauri    zote  hapa   Nchini  kila  mwaka  kwani  Halmashauri     nyingi  hapa Nchini   makusanyo  yao ya  dani   yanatofautiana  baina  ya  Halmashauri na  Halmashauri.
Alisema  kwa  sasa  Serikali imesitisha utoaji wa   urai kwa  Raia wa  Burundi kwa  ajiri ya kufanya uhakiki kwa wale waliopewa urai wa  Nchi ya  Tanzania  hivyo ni  vema kwa  wale  raia  wa   Burundi  ambao  hawaja  pewa  urai wakadhibitiwa kwa kutotoka  kwenye  makazi   mpaka  wawe  na  vibali.

Nae  Mkuu  wa  Mkoa wa  Katavi   Meja   Generali   Mstaafu  Raphael  Muhuga  alisema    Mkoa wa   Katavi  unachangamoto kubwa  ya   upungufu wa  watumishi wa   kada  mbalimbali  kwa kiwango cha  asilimia  35.
Muhuga  alifafanua kuwa  Sektarieti tuu ya  Mkoa huo  inao  upungufu wa watumishi kwa  asilimia 70 ya  watumishi wote  hari  ambayo  inasababisha  hari ya utendaji kazi kuwa  mgumu kutokana  na  idadi kubwa ya upungufu wa   watumishi kwa  ngazi ya  Mkoa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa