Home » » MADIWANI WA MANISPAA MPANDA WAMPONGEZA MAGUGULI WAWALANI VIKALI WANAOMBEZA.

MADIWANI WA MANISPAA MPANDA WAMPONGEZA MAGUGULI WAWALANI VIKALI WANAOMBEZA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma .
      Katavi .
Madiwani wa  Manispaa ya  Mpanda  Mkoani  Katavi  wametowa tamko la  kumpongeza  Rais  John Magufuli  kwa ujasiri   aliouonyesha  wa kulinda  rasrilali za  Nchi  hasa  katika swala la madini na wamawalaani vikali Watanzania  wanaobeza   jitihada hizo   zinazofanywa .
Tamko  hilo  la  madiwani lilitolewa  hapo jana  mbele ya Wandishi wa  Habari  na  Meya wa Manispaa ya  Mpanda  Willy  Mbogo kwa niaba ya  Madiwani  wote wa Manispaa ya  Mpanda.
Mbogo  alisema  Madiwani wa  Manipaa ya  Mpanda  wanatowa tamko la  kumpongeza   Rais  John  Magufuli  kwa ujasiri mkubwa  aliouonyesha  wa kulinda   rasilimali za   nchi  yetu   na  hasa   katika  suala  zima la  madini .
 Alisema  wanawalaani  vikari  Watanzania  ambao  wanaobeza  jitihada  hizo  zinazofanywa  na  Rais  za kulnda  rasilimali zetu za  Nchi  za  Madini  kwa  ajiri ya  manufaa ya  Wanzania  wote .
Alieleza   kuwa Rais  mwanzo  aliunda   kamati mbili   ambazo  zilitowa taarifa  na  sasa   amezifanyia kazi  mapendekezo  yaliotolewa na  kamati hizo  na  tayari   tumeanza kupata manufaa  kwani  Kampuni   ya    BARICK    GOLD  imekubali  kutupatia  ailimia 16 ya hisa  za   kampuni yao .
Na  pia  wamekubali kulipa   Dola   milioni  mia  tatu  na kugawana  nusu kwa nusu  faida ya  mapato  yanayopatikana  kitu  ambacho kimetokana  na  jitihada za  Rais  wetu za  kulinda  rasilimali za  Nchi  yetu .
 Alisema   Madiwani wa  Manispaa ya  Mpanda  wanaamini  mapato hayo  yatakayopatikana  yataiongezea  Serikali   mapato  na  Halmashauri  zitaongeza uwezo  wa kutowa huduma kwa  Wananchi wake .
Diwani wa  Kata ya  Makanyagio  Haidari  Sumry aliomba kuwa  swala hilo  lisiishie kwenye swala la  madini tuu   bali nguvu iongezeke kwenye  maeneo  mengine  ili  uchumi wa  nchi  uweze  kukuwa  na kuongezeka zaidi ya sasa.
Alisema  endapo rasilimali za  nchi    zitasimamiwa  vizuri   Halmashauri zitanufaika  na  pato  litakalokuwa limeongezeka  Serikali  kwani   hata  huduma  kwenye  Halmashauri zitaboreshwa zaidi .
Getruda  Kabinda   Diwani wa  viti  maalumu  alisema  kuna watu  ambao walikuwa wakinufaika  na  ndio   hao wanaobeza na kupinga jitihada  zinazofanywa na  Serikali za  kulinda  rasilimali za   Nchi kwa   faida ya  Wanzania wote.

MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa