Home » » JELA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI MWENE UMRI WA MIAKA 9

JELA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI MWENE UMRI WA MIAKA 9

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma .
        Katavi .
Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoani   Katavi  imemuhukumu  Lazaro   Peter  Ngomalala  50  Mkazi wa  Kijiji cha  Simbwesa    Wilaya ya  Tanganyika  kifungo cha  maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka   mtoto wa  miaka tisa jina  limehifadhiwa  mwanafunzi wa    darasa la  pili wa   Shule ya  Msingi  Simbwsa.
Hukumu  hiyo ilitolewa  jana  na  Hakimu   Mkazi    Mfawidhi wa  Mahakama ya Wilaya ya  Mpanda  Chiganga  Ntengwa  baada ya kuridhika na ushahidi wa  mashahidi  sita  wa upande wa mashitaka  akiwemo  mwanafunzi huyo  aliyebakwa  uliotplewa  Mahakani .
  Kabla ya kutowa   hukumu  hiyo Hkimu  Ntengwa  alisema  mtu   yoyote  anaefanya kitendo  kama  alichofanyiwa   mtoto huyo  anakuwa  amrfanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha   sheria   namba 130 kifungo kidodo cha kwanza na cha pili na  na kifungu    cha  sheria namba 131  kifungu kidogo cha  tatu cha  kanuni ya  adhabu .
Alieleza kutokana  na  ushahidi uliotolewa   Mahakamani  hapo na  upande wa  mashitaka akiwemo  mtoto mwenyewe na    mtoto mwenzake  ambae  alishudia   tukio  hilo  Mahakama  pasipo  shaka  yoyote imemwona  mshitakiwa   Lazaro  Ngomalala kuwa    anayohatia .
Ntengwa  alisema  miuongoni mwa  ushahidi wa sababu zilizoifanya   Mahakama   imtie  mshitakiwa  hatiani ni  ushahidi  uliotolewa mahakani na  mtoto alibakwa  na  mtoto mwenzake mwenye umri wa miaka saba  licha ya kuwa na umri mdogo  walitowa ushahidi  kwa ufasaha  mkubwa juu ya tukio hilo.
Pia  Mahakama  ilijiridhisha na  ushahidi uliotolewa  na   muuguzi wa  Zahanati ya  Simbesa  alimfanyia  uchunguzi  na kubaini i kuwa  mtoto  huyo  alikuwa  amembakwa  hari  ambayo ilimlazimu muuguzi huyo  amwanzishie  dawa ya kuzuia   maambukizi ya  VVU.
  Kabla ya  kusomewa  hukumu  hiyo  hakimu Ntengwa  alitowa  nafasi  kwa  mtuhumiwa   Lazaro  kama  anayosababu ya msingi   ya  kuishawishi  mahakama  iweze kumpunguzia  adhabu hivyo  mshitakiwa  aliiomba  Mahakama  imwachie  huru kwa kile   alichodai  kuwa  yeye  hakutenda kos  hilo  bali   amesingiziwa na  mama  mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa  alikuwa akimdai  fedha  alizokuwa   anamdai   baada ya kumkopesha.
Baada ya  utetezi huo  wa  mshitakiwa   Hakimu    Chiganga  Ntengwa  alisema kutokana   na  mshitakiwa  kupatika  na  hatia   ya  kifungu  cha   sheria    namba  131 kifungu  kidogo cha     cha tatu  kinachoeleza mtuyoyote  atakae   mbaka   mtoto  mwenye  umri wa  chini ya  miaka  kumi  adhabu yake ni kifungo cha maisha  jela .
  Hivyo kutokana  na  mshitakiwa   Lazaro  Ngomalala  kupatikana  na  kosa  hilo  Mahakama imemuhumu kuanzia  jana  kutumkia  jela  kifungo cha  maisha   jela .
Awali  kwenye  kesi  hiyo    Wakili wa  Serikali   Fravian  Shiyo  alidai   Mahakamani  hapo kuwa   Lazaro alitenda kosa  hilo  hapo   Oktoba  12  mwaka  jana  majira ya saa  nne  asubuhi kijiji   katika  Jijiji  cha  Simbesa.
 Ilidaiwa kuwa  siku  hiyo ya  tukio  mshitakiwa   alikuta  mtoto   aliyemtenda  kitendo  hicho  akiwa na  mtoto  mwenzake wakiwa   wanacheza  jirani na  nyumba yao ndipo  alipowadanganya wafuate  nyumbani kwake  iliakawapatie   fedha za kununulia  biscuit na  soda .
  Shiyo  alieleza kuwa  wakati wakiwa   wanaelekea  nyumbani kwa   mshitakiwa     walipofika  kwenye  eneo la  tanki la  maji  Lazaro  alivuta kwa  nguvu mtoto  huyo na  kuanza  kumbaka  licha ya mtoto huyo kubiga  kelele  lakini  hakuweza kumwachia  mpaka  alipo  maliza  aja  yake .
  Mwanasheria    aliiambia  Mahakama  baada ya kufanyiwa  kitendo  hicho mtoto  huyo  alibakwa  alikwenda     kutowa  taarifa kwa wazazi wake  huku  akiwa  analia  na  baada ya   kutowa taarifa kwa wazazi wake     mtuhumiwa   alikamatwa  na   askari wa  mgambo wa  kijiji cha  Simbwesa na kisha  alifikishwa  katika kituo cha  polisi
MWISHO



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa