Home » » ALIYETAPELI AJIRA WATU 114 ATUPWA JELA

ALIYETAPELI AJIRA WATU 114 ATUPWA JELA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Imeandikwa na Peti Siyame, Mpanda
MKURUGENZI wa Shirika la Umoja wa Watu wa Afrika (APAPO), Kapeele Mpundililwa (36) amehuku
miwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Katavi kwenda jela miaka mitatu baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kujipatia kwa njia ya udanganyifu zaidi ya Sh milioni 3.9 .
Mkurugenzi huyo ambaye ni mkazi wa mjini Namanyere wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa alipatikana na hatia hiyo baada ya kuwatapeli watu 144 kuwa angewaajiri katika shirika hilo.
Hakimu wa mahakama hiyo Odira Amworo alitoa hukumu hiyo jana mjini hapa akisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka pasipo kutia shaka yoyote kwamba mshitakiwa alitenda uhalifu huo.
Hakimu Amwolo alieleza kuwa miongoni mwa ushahidi uliomtia hatiani mshitakiwa ni hati za waliotapeliwa ajira alizolipia kwenye benki, akaunti iliyokuwa ikimilikiwa na mshitakiwa mwenyewe ambazo ziliwasilishwa mahakamani kama kielelezo huku zikiwa na majina ya wote waliotapeliwa.
Awali, Mwendesha Mashtaka, Mwanasheria wa Serikali Peter Maiko alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Mei 23, mwaka huu kwa nyakati tofauti wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alifika wilayani Mpanda na kujitambulisha kuwa ni Mkurugenzi wa APAPO ambapo alianza kutangaza nafasi mbalimbali za ajira kwamba watakaofuzu wataajiriwa na shirika hilo.
Ilielezwa kuwa miongoni mwa njia alizozitumia kujipatia kiasi cha fedha hizo kwa udanganyifu aliwaagiza kila muombaji anayetaka kuajiriwa na shirika hilo lazima kwanza alipe ada.
Mwanasheria wa Serikali Maiko alidai mahakamani hapo kuwa kwa ngazi ya Mtaa na Wilaya muombaji alilazimika kulipa ada ya Sh 17,000 ili aweze kusailiwa huku sifa ikiwa lazima awe amehitimu elimu ya msingi hadi kidato cha nne huku katika ngazi ya mkoa ada ilikuwa Sh 160,000 na muombaji awe na stashahada.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alifanikiwa kuwatapeli watu 144 ambao wote walilipa jumla ya Sh milioni 3.9 ikiwa ni ada ili waweze kusailiwa na kuajiriwa na shirika hilo.
Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali, Maiko, fedha zote hizo ziliingizwa kwenye benki, akaunti ambayo namba zake walipatiwa waombaji na watu wanne waliokuwa wakimsaidia kazi mshtakiwa huyo. Ilielezwa kuwa baada ya mshtakiwa huyo kukamatwa wasaidizi wake wanne walitorokea.
CHANZO HABARI LEO 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa