Home » » AFISA MTENDAJI WA KATA AJIUA KWA KUJINYONGA KWA KUHOFIA DENI.

AFISA MTENDAJI WA KATA AJIUA KWA KUJINYONGA KWA KUHOFIA DENI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 




Na  Walter  Mguluchuma .
     Katavi .
 Afisa  Mtendaji wa  Kata ya  Litapunga  Tarafa ya  Ndurumo  Wilayani  Mpanda   Agustino    Wangabo 53    Mkazi wa   Mtaa wa    Airtel  Kata ya  Uwanja wa  Ndege  Manispaa ya Mpanda  amejinyonga  hadi  kufa  juu ya paa la nyumba yake  kwa kutumia  mkanda wake  wasuluali  kwa kisa cha kufofia  deni.
  Tukio hilo la kujinyonga  kwa  mtendaji huyo wa  Kata  lilitokea  hapo  jana   majira ya saa  saba  mchana  nyumbani  kwake  na  Marehemu   katika  Mtaa wa Airtel  Kata ya  Uwanja wa  Ndege  Manispaa  ya  Mpanda  Mkoani hapa .
  Diwani wa  Kata ya  Uwanja wa  Ndege   Stephano  Asalile   tukio  akisimilia  tukio   hilo   alisema   marehemu   kabla ya kuchukua  umamuzi wake wa kujinyonga    alikuwa akidaiwa  na   mtendaji  mwenzake wa  huko   Katumba  kiasi cha   Tshs    1,600,000 ambazo  alizichukua  toka  mwezi  Agosti mwaka huu  kwa lengo la kumuuzia  pikipiki   SANLG  ambayo  ilikuwa ni  mali yake  na   marehemu  Wangabo.
 Alisema  baada ya  mauziano  hayo ya pikipiki  marehemu   aliombwa  na   mteja wake   aweze   kumpatia  kadi ya  pikipiki  hata  hivyo  hakufanya   hivyo na   aliomba   apewe  pikipiki  hiyo kwa  lengo la  kwenda  nyumbani kwake kuchukua  kadi ya pikipiki  ili    aje   amkabidhi  mteja wake .
Asalile  alieleza   pamoja na marehemu  kuwa   amelipwa    kiasi  hicho  cha  fedha  hakuweza  kukabidhi  pikipiki   hiyo toka  mwezi   Agosti na   badala  yake    alitafuta   mteja  mwingine    na  kumuuzia  pikipiki  hiyo  na  baada ya  kuuza   hakuweza  kurejesha  fedha   alizokuwa  amechukua  kwa  mteja wake wa  awali .
Mtendaji  mwenzake  alianza kufanya  jitihada  za  kudai   arejeshewe  fedha  zake   lakini  marehemu     aliendelea  kumipiga   kalenda  mara  kwa  mara na    dalili za  kutorudishiwa  fedha  zake zilianza kuonekana .
  Alisema    hari  hiyo  ilimfanya    achukue  uamuzi wa  kwenda kutowa  taarifa  polisi  ndipo  hapo  jana  Mteja  huyo  alikwenda   akiwa  na  polisi  nyumbani kwa  marehemu kwa  lengo la  kufatilia  haki  yake wakati wakiwa  karibu   na nyumba ya  marehemu   walimuona  akiwa    barabarani  huku  akiwa   anakula  mandazi na  alipowaona  alitimua  mbio na kukimbilia  ndani ya  nyumba  yake .
Ndipo   polisi  alipoweza   kutafuta  uongozi wa  Serikali ya   Mtaa  kwa  lengo la  kufanya  upekuzi wa  kumsaka  ndani ya   nyumba  yake  na  walipoingia   ndani ya   chumba  chake waliweza  kumwona  marehemu  akiwa  juu ya  mtamba  wa  paa  lake  huku   akiwa    amejinyonga hadi kufa kwa kutumia   mkanda wake wa saluali.
Kamanda  wa   jeshi la  polisi wa  Mkoa wa  Katavi  Damas  Nyanda   amethibitisha  kutokea kwa  tuko la  kifo  hicho  cha   mtendaji wa  Kata ya   Litapunga   ambacho   alisema  kimetokana  na    marehemu  kujinyonga kwa kutumia   mkanda wa suluali .
Mwili wa  marehemu  Agustino  Wangabo umehifadhiwa katika  chumba  cha kuhifadhi  maiti   katika   Hospitali ya   Manispaa ya   mpanda kwa   ajiri ya  kufanyiwa  uchunguzi .
MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa