Home » » WAVAMIZI 30 WAMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA

WAVAMIZI 30 WAMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  WAVAMIZI 30 wamehukumiwa  kifungo cha mwaka mmoja jela  na  Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi  baada ya kukiri  makosa matano yaliyokuwa yakiwakabili   ya kuishi  kinyume cha Sheria ndani ya Hifadhi ya Luangwa River  licha ya kutimuliwa  mara kwa mara .

Makosa mengine waliyokuwa wakikabiliana nayo ni pamoja kujenga  , kukata miti , kulima  na kusihi bila ya kibali ndani ya hifadfhi hiyo .

Hakimu wa mahakama hiyo , Teotimus Swai aliwahukumu washtakiwa hao kila mmoja kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukiri makosa yao .

Akihukumu alisema kuwa licha ya washtakiwa hao kutoisumbua mahakama kwa kukiri makosa yao  lakini amelazimika kuwapatia adhabu kali ili iwe fundisho kwa  wengine wenye tabia kama zao .

Awali  Mendesha Mashtaka , Bakari Hongoli  alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao  ikwa nyakati tofauti mwaka huu walitimuliwa kutoka  hifadhini  na kuamriwa na  Mkuu wa Wilaya ya Mlele , Rachael Kasanga kutorejea tena hifadhini.

Ilielezwa mahakamani  hapo kuwa lakini washtakiwa hao walikuwa wakikadi  amri hiyo halali ya Mkuu wa Wilaya  na  kurejea hifadhini  huku wakiendelea kufanya shughuli za kibinadamu ambaoz hazikuwa endelevu .
Mwisho  

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa