Na Walter Mguluchuma.
Katavi.
ZAIDI ya kaya 200 katika kijiji cha Ipota katika kata ya Ikuba katika
wilaya ya Mlele mkoani Mlele hawana makazi ya kuishi baada ya nyumba
zao kuteketezwa kwa moto na askari wa Shirika la hifadhi za mbuga za
Taifa (Tanapa) na askari polisi kwa madai kuwa sio makazi rasmi.
Tukio hilo la lilizua taharuki kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho
ambapo wa siku mbili mfululiozo kaya hizo , wakiwemo watoto ,
wanawake na wajawazito wanalazimika kulala chini ya miti cha huku
wakinyeshewa na mvua za masika . .
Inadaiwa kuwa askari wa Tanapa na askari polisi kutoka kituo cha
polisi cha Kibaoni katika wilaya ya Mlele waliteketeza nyumba za
wakazi hao kwa moto juzi .
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Ipota, Soguta Masanja Maduhu
akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hapo kiicho
jana alisema kaya 210ahazina makazi ya kuishi baada ya nyumba zao
kuteketezwa kwa moto na askari hao
“ Kaya zipatazo 210 hazina makazi ya kuishi baada ya nyumba zao
kuchomwa moto na askari wa Tanapa na askari polisi kutoka kituo cha
polisi kilichopo katika kijiji wilayani hapa (Mlele) na kusababishwa
kaya hizo kujibanza chini ya miti usiku kucha wakinyeshewa na mvua”
alisisitiza Masanja..
Akisimulia tukio hilo , Masanja alieleza kuwa askari hao
walifika kijijini humo juzi kwa kustukiza na kuteketeza nyumba
hizo kwa kuzichoma moto zoezi lililofanyika kwa siku mbili
mfululizo na kusababisha taharuki kubwa kwa wakazi hao .
“Kaya hizo zimepata mateso makubwa licha ya kuchomewa nyumba zao
bado askari hao waliwapiga wakazi hao ….hawakuwa na huruma kabisa
kwani waliwapiga watoto , wanawake , wajawazito na wagonjwa”
alieleza.
Alisema kumekuwepo na mgogoro mipaka ya makazi baina ya
TANAPA na wakazi wa kijiji hicho na Hifadhi ya Taifa ya
Katavi na eneo tengefu la kijiji na uhifadhi wa misitu na wanayama
pori “Wildlife Management Area” (WMA) kwa muda mrefu sasa .
Alifafanua kuwa nyumba hizo zilizoteketezwa kwa moto zinadaiwa na
Tanapa kujengwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
“Ukweli ni kwamba nyumba hizo zilijengwa mita 800 kutoka
Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwani utaratibu na sheria zilizopo ,
wananchi wanatakiwa kuwa kujenga makazi yao umbali wa mita 500
nje ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi na mita 300 nje ya WMA na
wakazi hao walifanya hivyo “ alisisitiza ..
Aliiomba uongozi wa serikali ya mkoa wa Katavi wafike kijijini
hapo ili kupima mipaka ya kutoka kwenye Hifadhi ya Taifa ya
Katavi hadi kwenye makazi ya kijiji hicho ili ndipo
ukweli ujulikana kwa kuwa wao wana uhakika eneo hilo wanalo ishi
liko nje ya hifadhi hiyo .
Kwa upande wake Joseph Kalubwa alisema mipaka
inayotenganisha hifadhi hiyo na kijiji hicho ni ya asili .
Nae mkazi wa kijiji hicho ,Samwel Kisinja alidai familia yake
yenye watu wapatao 32tangu juzi wamelazimika chini ya miti usiku
kucha baada ya makazi yao kuteketezwa kwa moto na askari hao ..
Mkazi mwingine , Maria Mchelu alisema mbali ya kuchomewa na
nyumba yake pia askari hao waliteketeza kwa moto magunia
yake matatu .
Hadija Madilisha aliiomba Serikali iingilie kati kunusuru maisha
yao huu wa mvua za masikaambazo zimeanza kunyesha mkoani humo
.
Nae Deus Kuhanda alisema wakazi hao wameishi kwenye kijiji
hicho kwa zaidi ya miaka 20
Mbunge wa Jimbo lao la Kavuu Dk
Pudensiano Kikwembe alisema kuwa taarifa za kuchomewa nyumba kwa
wananchi hao amezipata akiwa Bungeni Mkoani Dodoma hivyo
anawasiliano na uongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi ili
kuweza kujua ufumbuzi wa tatizo hilo la wananchi na hasa kwa
kutambua kwamba kipindi hiki ni cha masika.
0 comments:
Post a Comment