Home » » JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI LAKAMATA BUNDUKI SIRAHA ZA KIVITA AINA YA SMG , GOBOLE PAMOJA NA RISAS

JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI LAKAMATA BUNDUKI SIRAHA ZA KIVITA AINA YA SMG , GOBOLE PAMOJA NA RISAS


 Kamanda wa Polisi wa  Mkoa wa  Katavi Damas  Nyanda   akitowa  maelezo kwa  Wandishi wa  Habari  jana  ofisini  kwake  jinsi jeshi la  Polisi  Mkoa wa  Katavi lilivyofanikiwa kukamata  silaha    tano za  kivita  aina ya SMG   na  risasi  15 za  SAR  na  Bunduki  mbili  aina ya  Gobore  katika  kipindi cha  miezi mitatu kuanzia   Septemba   hadi   Novemba  Silaha  hizo na  risasi zilikamatwa  katika  Wilaya  za  Mlele  na  Mpanda .
Silaha    za  kivita  aina ya  SMG   na  risasi  15 za   bunduki  aina ya  SAR  pamoja  na  Gobore  mbili   ambazo  zimekamatwa  na  Jeshi la Polisi  Mkoa wa   Katavi katika  kipindi  cha  miezi  mitatu ya kuanzia  Septemba    hadi  Novemba  mwaka huu .
    Picha  na  Walter  Mguluchuma/Katavi yetu Blog

Na  Walter  Mguluchuma/
      Katavi yetu Blog

JESHI la Polisi mkoani Katavi  imekamata bunduki  risasi ita zikiwemo
SMG nne na risasi  15 za SAR.

Kamanda  wa  Polisi  wa  Mkoa  wa   Katavi  Damas  Nyanda alisema
silaha hizo zilikamatwa  katika msako maalumu uliofanyika katika
wilaya za Mlele na Mpanda mkoani huo katika  kipindi cha Septemba na
Oktoba

Alisema alisema Septemba 02, katika kijiji    cha  Kalovya ,   Tarafa
ya  Inyonga  katika wilaya ya Mlele watu wawili  ambao majina  yao
yamehifadhiwa  walikamatwa wakiwa  wanamiliki   bunduki  aina ya SMG
isiyokuwa  na   namba kinyume cha sheria  .

“Isitoshe   Septemba  28 ,   saa  mbili  usiku    lilifanikiwa mtu
anayeishi katika makazi ya  Wakimbi ya  Katumba  wilayani   Mpanda
ambae   jina    lake  nae  limehifadhiwa  alikutwa akimiliki  bunduki
aina  ya   SMG    yenye  namba   1954 KO  3927 PNB   na  risasi  15
za bunduki aina  ya SAR “alisisitiza

Alisema  tukio  jingine  lilitokea  hapo  Novemba  Mosi mwaka huu  saa
  12.30 osi  jioni   kijijini    Kamsisi katika wilaya   ya  Mlele
mtu  mmoja  ambae  hakufahamika   alisalimisha   bunduki   aina ya
SMG    yenye  namba     1953MM  3468   kwa  kuitupa  nje ya   mlango
wa  nyumba ya  Mwenyekiti wa  kijiji  hicho .

 Siku  hiyo  hiyo   huko  katika  Kijiji  cha   Utende    Tarafa ya
Inyonga   mtu   asiye  fahamika   alisalimisha  bunduki   aina  ya
SMG yenye   namba  0957  ikiwa  na   magazine   moja  isiyokuwa  na
risasi  wala mtu  huyo  aliyesalimisha  silaha  hiyo  hakuacha  ujumbe
 wowote wa   maandishi “alisema .

 Kamanda   Nyanda   alisema Novemba 02  katika  kijiji  cha  Itenka,
Ofisa  Mtendaji wa  Kata ya  Itenka   wakati  akiwa  afisini  kwake
alifika  Mwenyekiti wa  Kitongoji   cha   Kaderema  akiwa  na   silaha
iliyotengenezwa  kienyeji ‘gobori”   ambayo  ilisalimishwa  na   mkazi
wa kijiji   hicho   ambae  alikuwa   akisakwa na  Polisi   kwa kuhofia
kukamatwa na    silaha  hiyo   alimpa  mkewe   ndio  aikabidhi kwa
Mwenyekiti wa Kitongoji   na  yeye kutokomea  kusiko julikana .

Kwa mujibu  wa  Nyanda   katika  kijiji  cha   Mtakuja    Kata ya
Nsekwa  mtu  mmoja  alisalimisha   bunduki   aina ya  gobori   kwa
Mwenyekiti wa  kijiji  hicho  na   kueleza  nia  yake  ya kuachana na
 kufanya  ujangili  huku    akiwa   ameambatanisha   na  risti
aliyolipia   silaha  hiyo   ya  mara ya  mwisho  yenye thamani ya Sh
3,000 -  mwaka 2007  katika  Halmashauri ya  Wilaya ya   Mpanda .

Kamanda  Nyanda  aliomba   jamii  kuendelea  kushirikiana   na   Jeshi
 la  Polisi   katika  kutoa   taarifa   za  uhalifu  na   wahalifu
kwani  lengo kubwa  ni  kuona   kwamba  mkoa huo   unakuwa  salama
zaidi .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa