Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Watu wawili wamefariki Dunia hapo hapo na wengine 11 kujeruhiwa na kulazwa Hospitalini baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mpanda kwenda Tabora kupinduka baada ya kucha njia .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia wandishi wa Habari jana kuwa ajari hiyo ilitokea hapo jana majira ya saa nane mchana huko katika eneo la mlima Kanono Wilayani Mlele barabara itokayo Mpanda kuelekea Tabora .
.
Aliwataja marehemu hao wawili walikufa hapo hapo kuwa ni Hilika Maswalo mwenye umri wa miezi mitatu Mkazi wa Kijiji cha Mwamapuli Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na mtoto mmoja mwenye mwenye umri wa mwaka mmoja ambae amefahamika kwa jina moja Baluhu Mkazi wa Tabora
Ajari hiyo ilisababishwa na basi hilo kukatika breki wakati likiwa linashuka kwenye mlima na kasha liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watoto hao wawili na kujeruhi watu 11.
Kamanda wa Polisi Nyanda alisema ajari hiyo ililihusisha basi lenye Namba za usajiri T 258 DZD aina ya Scania mali ya Boazi Kemeu Mkazi wa Mwanza la Kampuni ya BMK lililokuwa likiendeshwa na John Sadock Mkazi wa Mkoa wa Tabora ..
Bsi hilo la Kampuni ya BMK lilikuwa likifanya safari kutoka Mjini Mpanda Mkoani Katavi na kuelekea Mkoani Tabora kupitia Wilayani Mlele Mkoani hapa .
Alisema katika ajari hiyo watu 11 walijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Inyonga huku wanawake wakiwa saba na wanaume wane na kasha majeruhi wanane walipewa rufaa na kuhamishiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambapo wamelazwa na wanaendelea kupatiwa matibabu .
Hari ya majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda wanaendelea vizuri na wale watatu walilazwa katika Hospitali ya Inyonga wanaendelea vizuri
Dreva wa basi hilo anashikiwa na Polisi na anatarajiwa kufikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi wa ajari hiyo utakapo kuwa umekamilika .
0 comments:
Post a Comment