Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mkoa wa Katavi Mselemu Abdala amewagiza Makatibu wa CCM wa Wilaya zote za Mkoa huu kuwachukulia harua mara moja wanachama wa Chama hicho ambao wameanza kufanya kampeni kwa ajiri ya kugombea Ubunge na Udiwani kwa ajiri ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.
Agizo hilo alilitowa hapo juzi wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele kwenye uwanja wa shule ya Msingi Inyonga Jimbo la Katavi .
Alisema wapo baadhi ya wanachama wa CCM ambao wameanza kufanya kampeni za kugombea Ubunge wa mwaka 2020 wakati ni kinyume na utaratibu wa Chama hicho .
Namnukuu wacheni viongozi walioko madarakani waendelee kufanya kazi kwenye majimbo yao kwani watu kuanza kufanya kampeni kwenye majimbo yenye Wabunge mnawachanganya walioko madarakani sasa .
Aligiza kuwa Makatibu wote wa Wilaya wa chama hicho waakikishe kuwa wanawadhibiti watu wote ambao wameanza kufanya kampeni kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi katika Mkoa wa Katavi .
Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Katavi Mselemu Abdala alieleza kitendo cha watu kuanza kufanya kampeni wakati huo kutawafanya viongozi wa majimbo hayo kushindwa kufanya kazi zao vizuri .
Alisema wakati huo sio kipindi cha kufanya siasa bali ni wakati wa kufanya kazi anae taka siasa asiburi hadi mwaka 2020 ndio muda wa kufanya siasa .
Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa CCM alitowa agizo hilo baada ya kuwepo kwa taarifa za kuwa kuna mwanachama mmoja ameanza kufanya kampeni katika jimbo la Katavi linaloongozwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng Izack Kamwelwe kwa ajiri ya uchaguzi wa mwaka 2020 .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mlele Lechor Kasanda alieleza kuwa Wilaya hiyo imeisha anza mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa , nyumba za kuishi walimu na ujenzi wa vyoo bora vya kisasa .
Alisema anatowa wito kwa Wananchi kuunga mkono jitihada hizo za Serikali ya Wilaya hiyo kwa wananchi kuchangia michango mbalimbali ilikuweza kufanikisha ujenzi huo .
Dc huyo alieleza kuwa Serikali ya Wilaya hiyo imewaagiza wananchi wa Wilaya hiyo kuhakikisha kwa kipindi cha miezi mitatu kuwa kila mmoja we amejenga choo bora na cha kisasa kwenye nyumba yake na baada ya kupita kipindi hicho timu ya wataalamu wa afya watapita kwa ajiri ya ukaguzi na watakao kuwa wamebainika kushindwa kutekeleza agizo la kuwa na choo bora na cha kisasa watachuliwa hatua alisema Dc Kasanda
0 comments:
Post a Comment