Home » » SERIKALI KUJENGA BARABARA ZA RAMI KUUNGANISHA KATAVI NA MIKOA MINGINE.

SERIKALI KUJENGA BARABARA ZA RAMI KUUNGANISHA KATAVI NA MIKOA MINGINE.


    Na  Walter  Mguluchuma .
       Katavi yetu Blog
  Serikali ya  Jamhuri ya  Muungano wa  Tanzania imepanga   kutengeneza  barabara   kwa  kiwango  cha   Rami  zitakazo  uunganisha  Mkoa  wa  Katavi na   Mikoa  mingine inayopakana  na   Mkoa  huo .
  Kauli  hiyo ya  Serikali  ilitolewa  hapo  juzi  na  Waziri  Mkuu  Kassimu  Majaliwa  wakati   alikuwa akiwahutubia  Maefu ya  Wanachi  wa  Kata  ya  Majimoto  Wilayani   Mlele  kwenye   uwanja wa  Maji  moto.
Majaliwa  alisema   Mkoa  wa    Katavi  upo  kwenye   mpango  wa  kuunganishwa  na  mikoa  mingine  kwa  barabara  zake   zote   zina zinazoungana  na  Mkoa   huo  kutengenezwa kwa kiwango cha    lami .
 Alizitaja   barabara  hizo kuwa  ni  Mpanda   Sumbawanga ambayo  teyari ujenzi wake  umeishaanza ,Mpanda     Tabora  ambapo  taratibu za kuwapata  wakandarasi  zimeanza kufanyika   na  Mpanda   Uvinza  ambapo   mkandarasi wa kutengeneza  kilometa  32  za  kuanzia    Mpanda  kuelekea  Uvinza  Mkoani   Kigoma  amekwisha  patikana na   anatarajia  kuanza  kazi   hivi  karibuni .
  Waziri  Mkuu   Majaliwa   aliwaeleza   Wananchi  hao  kuwa   kwa  sasa   Serikali ya  Tanzania  inayo inazo  fedha za kutosha  baada  ya  kuwabana  mafisadi  na  wafanya  biashara   ambao  wanao  kwepa  kulipa   kodi .
  Hari  hiyo ya  ukusanyaji  mkubwa wa   mapato ya   Serikali   imefanya   Serikali   ipange  mipango yake ya  maendeleo    vizuri kutokana  na  kodi  mbalimbali  zinazokusanywa .
  Alieleza  kuwa   Serikali  imepanga  pia kujenga  Reli itakayotoka  Mpanda   hadi   Karema  kwa  lengo la  kufarisha  mizigo   kwa  njia ya  Treni  kutoka   Tanzania   hadi   Kongo kwa kupitia     bandali  ya   Karema   katika  ziwa  Tanganyika .
  Pia  alisema   Serikali  inampango  wa   kufungua  furusa  za  utalii  katika   Mkoa wa  Katavi   na   ndio   maana  wanatengeneza  miundo mbinu ya  uhakika  ili  watalii waweze  kufika  huku kwa  urahisi .
 Nae   Mbunge wa  jimbo  la   Kavuu  Dk  Pudensiana  Kikwembe  aliiomba  Serikali   iweza   kuwapatia  wanachi  wa  jimbo  hilo  maji safi  na  salama kwani  robo  tatu ya  wananchi wa  jimbo  hilo   hawapati  huduma ya   maji .
Alisema  hata  hao  roba  ya  wakazi  wa  jimbo  hilo  wanao  pata   huduma  ya  maji  sio  safi  wala   salama  hari  ambayo  imekuwa  ikiwasababishia  kupata  mlipuko wa  magonjwa  mbalimbali .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa