Home » » PINDA ACHENI KUGOMBEA MALI ZA MAREHEMU

PINDA ACHENI KUGOMBEA MALI ZA MAREHEMU


   Na  Walter  Mguluchuma
         Katavi.
  Waziri  Mkuu   msitaafu  Mizengo  Pinga   ameitaka  jamii  ya  Kitanzania  kuachana  na   mila   potofu  za  wanandugu  kugombania  mali  za  marehemu  bali    i waziache  ili  zitumiwe  na  mke wa  marehemu  na  watoto  aliowaacha  marehemu .
  Pinda  aliyaeleza   hayo  juzi  wakati  wa  mazishi  ya  aliyekuwa  Diwani wa  Kata ya  Kasansa    Halmahauri ya  Mpimbwe  Wilaya  ya  Mlele   Sixto  Chalahani  yaliofanyika   juzi  katika  Kijiji  cha  Kasansa  Tarafa  ya  Mamba .
 Alisema kuwa  ndugu wa   marehemu   wanapaswa  kuachana  na  utamaduni  huo wa  kugombania  mali  za  marehemu  ambao   unasababisha   mjane wa marehemu  na  watoto  kuhangaika   badala  yake  kuhakikisha   watoto  walioachwa  na  marehemu   wanaendelea  na  masomo    hata  kama  mali  hizo  zitakuwa zimekwisha    jamii iendelee  kusaidia  familia  hiyo .
 Alifafanua  kuwa  jamii ya  kabila  la  Wapimbwe  analotoka  yeye  Pinda   mme  anapofariki  wanautamaduni  wa  ndugu  wa  upande  wa  mme kugawana  mali  za  marehemu  na  kuwaacha   mjane   na  watoto  wa  marehemu  na  kuwaacha   mjane  na  watoto  wa  marehemu  kuhangaika   mitaani   hatimae  kwa  waliokuwa  wakisoma  kushindwa  kuendelea  na  masomo .
  Wakati  huo  huo   Pinda   aliwataka   wananchi   wa  Kata  hiyo  kuanza   kujiandaa  na  uchaguzi  mdogo  kwa  kufikilia   nani   atakuwa  Diwani  wao   bora  atakae weza  kuendeleza   aliyoacha   marehemu    Sixto  Chalahani  katika  kipindi  hiki  kilicho  baki .
 Marehemu   Sisto   alikuwa ni  Diwani wa  Kata ya Kasansa  toka  mwaka   2010  hadi  hapo  mauti yalipomkuta   tarehe    23 Agosti huko   Sumbawanga  katika   Hospitali ya     Mkoa  wa Rukwa  alikokwenda  kupatiwa  matibabu .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa