Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Gaeorge Mbijima amewataka Watanzania kuwapuuza viongoz wa vyama vya siasai wanaowapotosha wananchi kuwa Mwenge wa uhuru ni wachama kimoja cha siasa washauliwe wakatibiwe Milembe Hospitali
Kiongozi wa mbio za mwenge alitowa kauli hiyo hapo jana wakati alipokuwa akiwatutubia wananchi wa Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi kwenye uwanja wa shule ya msingi Inyonga mara baada ya kukabidhiwa risala ya itii kwa Rais kutoka Wilaya ya Mlele .
Alisema wapo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakiwapotosha watu kuwa mwenge wa uhuru ni wachama cha siasa wakati sivyo hivyo bali mwenge wa uhuru ni Wawatanzania wote .
Mbijimi alisema watu hao wanaoubeza mwenge ni vizuri wakashauliwa waende hospitali ya Milembe Dodoma kwa ajili ya kutibiwa kwani lazima watakuwa na ugonjwa ambao matibabu yake yanapatikana Milembe.
Alifafanua kuwa ni vema watu wakatambua kuwa mwenge wa uhuru sio wa Cuf,, CCM, CHADEMA , ACT wala chama chochote cha siasa mbali ni mali ya watanzania wote bila kujali itikadi za vyama wala dini yoyote.
Pia aliwataka Watanzania kuwaepukana na watu ambao wanataka kuwabagua Watanzania kwa itikadi za vyama na dini bali watambue kuwa watanzania wote ni wamoja .
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge alizitaka Halmashauri zihakikishe fedha zinazotengwa kwa ajiri ya vijana zinawafikia kama ilivyopangwa na sio vinginevyo.
Jumla ya miradi ya maendeleo kumi na mbili yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.05 ilizinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
0 comments:
Post a Comment