Na Walter Mguluchuma.
Katavi.
Mwenge wa Uhuru umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya zaidi ya shilingi Bilioni 2.05 wakati wa mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi huku zaidi ya shilingi milioni 300. 3 zikiwa ni fedha za kutoka kwa wahisani na Shilingi milioni 412 fedha za kutoka katika Halmashauri hiyo huku Serikali kuu ikitowa zaidi ya shilingi Bilioni 1.6
Hayo yalisemwa hapo jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mlele Epherance Tenganamba wakati alipokuwa akisoma kiapo cha utii kwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania cha Wilaya ya Mlele mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge George Mbijima kwenye uwanja wa shule ya Msingi Inyonga .
Jumla ya miradi 12 ilizinduliwa wakati wa mbio hizo za mwenge kati ya miradi hiyo miradi mitatu iwekwa mawe ya jiwe na msingi na kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa .
Kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 1.6 ziritoka serikalini kuu shilingi milioni 412 kzilitoka Halmashauri wahisani walichangia shilingi milioni 333 na wananchi walichagia shilingi milioni 25.
Tenganamba alieleza mwaka jana kwenye Halmashauri hiyo Mwenge wa uhuru ulizindua miradi na kuweka maawe ya msingi kwenye miradi iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 913 ambapo Serikali kuu ilichangia kiasi cha shilingi milini 544 Halmashauri shilingi milioni 263.2 na wahisani walichangia kiasi cha shilingi milioni 100.
Aliitaja miradi iliyowekewa jiwe la Msingi mwaka huu kuwa ni ujenzi wa nyumba tano za kuishi waalimu wa shule za Kata ya utende , ujenzi wa nyumba tano za kuishi watumishi wa Halmashauri ya Mlele na ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali tarajiwa ya Wilaya ya Mlele .
Baadhi ya miradi iliyozinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa ni ofisi ndogo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Dirisha la kutolea dawa kwa ajiri ya wazee katika hospitali tarajiwa ya mlele ambayo ilijengwa kama kituo cha afya barabara ya lami yenye urefu wa kilometa mbili kuzunguka mji wa Inyonga pamoja na kituo cha michezo ambacho kinatumika pia kwa ajiri ya kuwaelimisha vijana waache kutumia dawa za kulevya .
Nae Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Geoge Mbijima aliwaka Wanzania wasidharauliane kwa ajiri ya itikadi za siasa wala dini .
Pia watu wawaheshimu viongozi walioko madarakani nao viongozi wawatumikie vizuri watu wanao waongoza bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa .
Mbijima aliwaasa vijana kuwa na tabia ya kufanya kazi na wawe wanachangia maendeleo ya Taifa badala ya kuwa wanajihusisha na matukio ya uharifu na dawa za kulevya kwani serikali ya awamu ya tano inataka mabadiliko kwenye kila sekta .
Alizita Halmashauri kuhakikisha kila kinachotakiwa kuwafikia vijana kutoka katika Halmashauri kina wafikia na vijana wajiunge kwenye vikundi ili waweze kunufaika na mikopo itakayokuwa ikitolewa kwenye Halmashauri zao .
0 comments:
Post a Comment