Home » » WAMILIKI WA AICE WAGOMA WAKIWAHUTUMU TRAFIKI KUWATOZA FEDHA ZA BOOK SAFARI.

WAMILIKI WA AICE WAGOMA WAKIWAHUTUMU TRAFIKI KUWATOZA FEDHA ZA BOOK SAFARI.


    Na  Walter   Mguluchuma   Na  Arine Temu .
         Katavi .
 Wamiliki na   madreva  wa Aice wanaofanya  safari zao za kusafirisha  abiria  katika   stendi kuu ya  Mpanda  Mkoani  Katavi wamegoma kufanya  safari zao hapo  jana kwa kile wanachodai kuchoshwa na fedha  wanazotozwa na  Askari wa  usalama  barabarani  zinazoitwa  safari Book kila waondokapo, na wanapokuwa  njiani  na  kwenye kituo wanachoishia  safari .
  Wamiliki na  madreva waliogoma ni wale  wanaofanya  safari zao  kwenda  Ugala , Inyonga  Wilaya ya  Mlele , Ikola na Vikonge Wilaya ya Tanganyika  pamoja   na  Kakese  Mwamkulu Manispaa ya  Mpanda .
 Baadhi ya  wamiliki  hao waliwaambia  wandishi wa Habari jana  kwenye   stendi kuu ya  Mpanda kuwa hawako  tayari  kufanya  safari zao   mpaka  hapo  askari wa usala  barabarani watakapokuwa  wamewaondolea malipo   yasiyotambulika wanayoyaita Book  safari  ambapo wamekuwa wakizwa kwenye kituo cha ofisi ya usama  barabarani iliyoko  katika   Stendi  hiyo .
  Mmoja wa   wa wamiliki wa  Aice inayofanya   safari zake toka   Mpanda  kwenda  Ikola   Daudi  Kiula  alisema wamekuwa wakitoozwa kiasi cha   Tsh   5,000 kila wanapotoka  kwenye   stendi kuu na wanapofika  kwenye  kituo cha kukaguliwa  wanatozwa   tena  Tsh 5,000 na wanapofika  kwenye kituo cha mwisho wamekuwa wakitozwa  tena  Tsh 5,000.
  Hivyo kwa  safari  moja  wamekuwa  wakitozwa  Tsh  15,000 kwa  safari ya kwenda na kurudi wamekuwa wakitozwa kiasi  cha  shilingi  elfu  thelasini kwa kila  Aice  moja .
  Abeli  Kambaulaya  anae  fanya  safari  zake  Mpanda  .inyonga   alisema  kuwa  fedha  hizo wanazotozwa  zimekuwa ni  kero  kubwa   sana  ndio  maana   tumeamua tusitishe  safari zetu    mpaka  hapo  tutakapo  elezwa  kama  kweli   malipo   hayo  yapo kwa  mujibu wa   sheria .
Kwa  upande   John   Mwananyama  ambae ni  mkatishaji wa  tiketi ya  Aice  inayofanya  safari zake  kwenda  Ugala  Wilayani  Mlele  aliwaambia  wandishi wa   habari wamekuwa wakipewa  fomu na  askari wa usalama  barabarani  inayoitwa   Book  safari  ambayo  huwa wanajaziwa  kila wanapolipia wanapo kuwa wanaondoka na wasipofanya hivyo huwa wanatozwa  faini ya Tsh  30,000.
Fomu  hiyo wanayojaziwa  kila  wanapokuwa kuwa wamelipia  haina  hata  nembo yoyote  ile ya  Serikali   embu  tazameni  hata  nyie  Wandishi wa  Habari   alisema   huku   akiwa   anaonyesha  fomu  hiyo ya   boo  safari .
Mmoja  wa  abiria   Salome  John  alisema   yeye  ameshuka  leo  yaani   jana  na   treni akiwa   anatoka  Mwanza kwa kutegemea  angesafiri  kwenda   kwake  Ikola  lakini  kutokana   na  mgomo  huo  atalazimika  kulala  kwenye    stendi  kwani  hana  fedha za kulala  gesti kwani  hana   ndugu hapa    mjini   Mpanda .
Kamanda wa  polisi   wa  Mkoa wa  Katavi   Damas   Nyanda  alipotafutwa kwa  simu  yake ya  mkononi  hakuweza  kupatikana  ili  aweze kuelezea  ufumbuzi wa mgomo  huo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa