Home » » RAIS WA UTP C AWATAKA WANDISHI KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA.

RAIS WA UTP C AWATAKA WANDISHI KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA.


  Na  Walter  Mguluchuma.
   Katavi .
  Rais wa  Muungano  wa Klabu za Wandishi wa  Habari  Tanzani  UTPC  Deo  Nsokolo amewataka Wandishi wa  Habari hapa  Nchini   wajiunge  na   mfuko wa  Bima ya Afya  ili  waweze kunufaika na mfuko huo pindi wanapokuwa wameugua .
  Nsokolo alitowa kauli  hiyo  hapo  jana  alipokuwa  akizungumza na  Wandishi wa   Habari wa   Chama cha Wandishi wa  Habari  Mkoa wa  Katavi kwenye  ofisi za   Chama  hicho iliyopo  katika  Mtaa wa   Madukani   Mjini    Mpanda wakati wa ziara yake  .
Alisema umefika wakati R kwa kila Mwandishi wa  Habari  ambao ni wanachama  wa vyama vya wandishi wa  Habari vya  Mikoa na wale  ambao sio wanachama  wawekewe utaratibu  wa kujiunga na  Bima ya  Afya  kwani  inamanufaa sana pindi mtu  anapokuwa ameugua .
 Alifafanua kuwa wandishi wengi wa  Habari  kipato chao ni kidogo sana  hivyo watakapo kuwa  wamejiunga  na   Bima ya  Afya watapata manufaa ya kutibiwa kwa gharama  nafuu wao na watemezi wao .
Rais   huyo wa  UTPC    alisema ni  vema  vyama vya wandishi wa   Habari  vikawa na utaratibu wanapokuwa wanawapokea  wanachama wapi  wanaokuwa wanaomba kujiunga  na  vyama  vyao vya wandishi wa  Habari wakawekewa utara wa kuiunga  na Bima ya  Afya .
 Aidha  aliwataka wandishi    wajihadhari  wanapofanya kazi  wahakikishe wanafanya kazi  katika  misingi  ambayo    itawafanya wawe  salama   .
 Alisema wandishi wa  Habari  hawana nia  mbaya kwenye jamii  ila watu  wangine  wamekuwa  wamekuwa wakiwafikilia  vibaya  na  kutishia  usama wao .
MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa