Home » » MAFUTA YA PETROLI YAUZWA KWA BEI YA TSH 7000 BADALA YA TSH 2070 KWA LITA MOJA

MAFUTA YA PETROLI YAUZWA KWA BEI YA TSH 7000 BADALA YA TSH 2070 KWA LITA MOJA

.
 Na  Walter  Mguluchuma   Na  Arine  Temu
         Katavi yetu Blog
     Mji wa  Mpanda  Mkoani   Katavi  unakabiliwa  na  uhaba  mkubwa wa  mafuta ya   petrol kwa kipindi cha  siku tatu  mfululizo  na  kupelekea  lita  moja  ya  mafuta kuuzwa kwa   bei ya   shilingi  elfu saba   badala  ya   bei  elekezi ya  Tsh  2070 na  kupekekea  bei ya vyombo  vinavyo tumia  mafuta  hayo kupanda kwa  kiasi kikubwa .
 Wakiongea kwa  nyakati tofauti   na  gazeti   hili  wendesha  pikipiki  Bodaboda   wa vituo  mbalimbali vya  Manispaa ya  ya  Mpanda  walisema wanalazimika  kununua  lita  moja ya  mafuta kwa  bei ya    Tsh  7,000 kwa  lita  moja   badala ya  bei elekezi ya  Tsh 2070.
Mwenyekiti wa  bodaboda  wanaofanya   shughuli  zao  katika  kituo  cha   White   Club  Fericiani  Masanja  alieleza  kuwa  kwa  siku ya  tatu  mfululizo  vituo  vya kuuza  mafuta  vya   GBP   na  Allyen vikuwa  haviuzi mafuta ya  petrol kwa kile  wanachodai kuwa  mafuta  hayo yamekwisha mpaka  yaje  mengine  kutoka   Dares salaam.
  Alisema  kutoka  na  kukosekana  kwa  mafuta  kwenye  vituo  hivyo  wanalazimika  kununua   mafuta  hayo  mitaani kwa  bei ya  kuluka ya  Tsh  7,000 kwa  lita    moja  badala  ya  Tsh  2070 kwa lita  moja .
Boda  boda wa  kituo  cha  Soko  kuu la  Manispaa ya  Mpanda    Mawazo  Bacho  alieleza wamelazimika kupandisha  nauli mara  mbili kwa  sehemu walizokuwa wakiwatoza  abiria  nauli ya Tsh 2,000  sasa wanawatoza  Tsh  4,000.
Nae bodaboda wa  stendi ya  mabasi yaendayo  Mikoani  Liberatus Sigareti  alisema  mafuta    hayo  ambayo yamekuwa yakiuzwa mitaani  ani na wafanya  biashara wasio  rasmi yanaweza  kuhatarisha  usalama wa watu  kwani wakati wowote moto  unaweza kutokea  kwa jinsi  mafuta  hayo yalivyo hifadhiwa  kwenye  chupa  na   garoni  .
Mwenyekiti   wa   Chama  cha  bodaboda   Mkoa  wa  Katavi   Stephano  Asalile  alisema   toka  mji wa  Mpanda ukose   huduma  ya  mafuta ya  Petroli hari ya  uchumi  ya  boda boda imehathilika  kwani  boda  boda  waliowengi wamesimama  kufanya   shughuli   hiyo  iliyokuwa  ikiwaingizia  kipato .
 Alisema  hata  ukiangalia  mitaani wananchi  wamekuwa  wakipata  shida  sana  ya  kupata  usafiri   kutoka  na  uchache wa  bodaboda  zinazofanya  kazi  tofauti na  ilivyokuwa  imezowelela .
Asalile  aliiomba   Serikali ya  Mkoa  kuingilia   kati  tatizo  la  kukosekana  kwa  mafuta ya  Petroli  katika   Mji wa    Mpanda  kwani  limekuwa ni  tatizo la  mara  kwa  mara   alisema  mwenyekiti  huyo wa   chama  cha  Bodaboda   Mkoa  wa  Katavi
  Mkazi wa  Mtaa wa   Kawajense  Salome  Mwanandenje   alisema  toka  juzi   analazimika  kutembea kwa  miguu  kwenda kutafuta  mahitaji baada ya  kushindwa kulipia  nauli  aliyokuwa  ameizowea ya   Tsh  1,500 kutoka  kawajense  hadi soko kuu ambapo kwa  sasa   analazimika  kulipa  Tsh  3 ,000 kwa  safari moja tuu ya kwenda

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa