Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amewataka waandishi wa Habari kuwaelimisha jamii kuacha kukata miti ovyo ili kuweza kusaidia kuzuia uharibifu wa mazingira .
Mwamlima alitowa wito huo hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na wafanya biashara wenye viwanda vidogo vya kuchana mbao katika eneo la Pasifiki Mtaa wa Majengo B Manispaa ya Mpanda .
Alisema hari ya ukataji ovyo wa miti na uharibifu wa mazingira umekuwa ni mkubwa sana katika Mkoa wa Katavi na hari hiyo ikiendelea hivyo upo uwezekana mkubwa wa kutokea jangwa katika Mkoa huo ambao unasifika kuwa na uoto mzuri wa mistu kuliko mikoa mingine hapa Nchini .
Alisema ilikukabiliana na hari hiyo waandishi wa habari wanao wajibu mkubwa wa kuielimisha jamii kuacha tabia ya kukata miti ovyo ilikuinusuru Wilaya hiyo na Mkoa wa Katavi kuwa najangwa.
Mwamlima alieleza waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa ya kuelimisha watu umuhimu wa kutunza mazingira kutokana na nafasi yao walionayo kwenye jamii.
Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya uharibifu wa mazingira kwa kwa kukata miti ovyo ,kuchoma mapori na kufyeka ovyo mistu kutokana na kutokuwa na uwelewa wa kujua umuhimu wa kutunza mazingira.
Hivyo vyombo vya habari vione na vitambue vinaumuhimu sana wa kuwaelimisha watu kutunza mazingira yanayowazunguka kwenye vijiji vyao na kwenye mitaa yao
Alieleza swala la kuelisha jamii kutunza mazingira waandishi wa habari wasilione kuwa ni la serikali peke yao bali walione swala hilo ni jukumu lao.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema hari ya
uharibifu wa mazingira umekuwa ukiongezeka kwa kasi kubwa katika Wilaya
hiyo na mkoa kwa ujumla kutokana na watu kutoona umuhimu wa kutunza mazingira kitu ambacho ni hatari kwa Mkoa huu na Nchi pia.
0 comments:
Post a Comment