Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Serikali Wilayani Mpanda Mkoani Katavi imesitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti ya asili inayovunwa kwa ajiri ya mbao na magogo kutokana na kuwepo kwa uharibu mkubwa wa mistu katika Wilaya ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.
Agizo hilo lilitolewa hapo jana na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima wakati alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wenye viwanda vidogo vya kuchana mbao na kutengeneza vitanda na mirango ya mbao pamoja na samani za ofisi na nyumba kwenye eneo la Pasifiki Mtaa wa Majengo Mjini hapa.
Alisema kuanzia sasa Serikali ya Wilaya ya Mpanda imesitisha utoaji wa vibali vipya vinavyo waruhusu watu wavune miti ya mbao ya asili kutokana na uharibifu mkubwa ambao umefanywa wa uharibifu wa mistu katika Mkoa wa Katavi uliosababishwa na uvunaji holela wa miti ya mbao.
Mwamlima alieleza kuwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mistu unaoendelea kufanywa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi Serikali ya Wilaya hiyo imeamua kusitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti ya mbao na magogo na kwa wale ambao walipatiwa vibari hawata pewa tena vibali vingine mara baada ya vibali vyao vitakapo kuwa vimekwisha.
Alisema atakae kamatwa na mbao haramu afungwe na kupewa faini kubwa ili iwefundisho kwa watu wengine wanao fanya biashara haramu ya uvunaji wa miti ya mbao.
Atakae taka kibali cha kuvuna mbao atapewa kibali cha kuvuna miti ya kupanda na sio kuvuna miti ya asili kama ilivyo sasa hivyo wahakikishe wanapanda miti kwa ajiri ya kuvuna mbao .
Mkuu huyo wa Wilaya pia ameagiza mbao zote ambazo zilikamatwa zikiwa vimevunwa na wavunaji haramu zisipigwe mnada na zitumike kutengeneza madawati ya wafunzi .
Afisa Mistu Wilaya ya Mpanda Lucas Nyambala aliwataka wanye viwanda vidogo hivyo kuacha tabia ya kununua mbao kwa watu wasio na vibali badala yake wanunue kwa watu wenye vibali vya kuvuna mbao.
Mwenyekiti wa wenyeviwanda vidogo vya Pasifiki Sailoni Mhagama alieleza kuwa waharibifu wakubwa wa mistu ni wenye leseni kubwa na sio wenye leseni ndogo hivyo Serikali ya Wilaya ya Mpanda ingewapiga marufuku Raia wa Nchi ya China wanaofanya shughuli ya uvunaji wa magogo katika Mkoa wa Katavi kutokana na uharibifu mkubwa wanofanya wa kuharibu mistu .
Aliomba mbao zinazovunwa katika Mkoa wa Katavi zisiwe zinasafirishwa kutoka nje ya Mkoa huu ili watu wa Mkoa huu waweze kunufaika kwani mbao moja ya mti wa mninga inauzwa kati ya shilingi elfu kumi na nne na kumi na sita.
Nae Moshi Dede alieleza kuwa agizo hilo la kusitisha utoaji vibali vya uvunaji wa miti ya mbao ya asili utawaathili kwani miti ya kupandwa hutowa mbao zenye rangi nyeupe ambayo haipendwi na watu waliowengi.
0 comments:
Post a Comment