Home » » DC KAZI YA KUKUSANYA FEDHA ZA USAFI NI YAWATENDAJI WA MITAA NA SIO WENYEVITI WA MITAA

DC KAZI YA KUKUSANYA FEDHA ZA USAFI NI YAWATENDAJI WA MITAA NA SIO WENYEVITI WA MITAA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

           Na   Walter Mguluchuma
                  Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima amewapiga marufuku  wenyeviti wa Mitaa kujihusisha  na shughuli ya kukusanya usafi wa mazingira kwani jukumu hilo ni la maafisa watendaji wa Mtaa.
Mwamlima alitowa agizo hilo hapo jana wakati  wa kikao cha kamati ya  mashauliano  ya Wilaya ya Mpanda (DDC  kIlichofanyika katika ukumbi wa idara ya maji mjini hapa.
Alisema  kumekuwa na tabia  baadhi  ya wenyeviti wa mitaa kufanya shughuli ya kukusanya  fedha za usafi  wakati jukumu hilo ni la watendaji wa mitaa.
Alieleza  wenyeviti wa mitaa wao ni watu wakuchaguliwa  hivyo  kunauwezekano mkubwa  kwa wao kushindwa kuwakamata na  kuwachukulia hatua watu ambao wanaokuwa wameshindwa kulipa fedha kwa ajiri ya usafi wa mazingira kwa kuwa  waliwachagua kwa kuwapigia kura wakati wa uchaguzi.
Hivi karibuni DC huyo alifanya ziara katika Kata ya makanyagio  na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliowalalamikia wenyeviti wao kufanya shughuli za kukusanya fedha za usafi wa mazingira wakati watendaji wa mitaa wapo.
Nae Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mpanda Gervansi Nyaisonga aliwaeleza wajumbe wakikao hicho kuwa pamoja na kuwepo na mpango wa elimu bure bado  kunatatizo  la kundi kubwa  la watoto  wasio  soma shule  kutokana  na miundo mbinu.
Pia alishauli jina la Wilaya ya Tanganyika iliyotangazwa kuanzishwa hivi karibuni ni budi likabadilishwa na kuitwa jina la Wilaya ya ziwa Tanganyika kwani Tanganyika ilikuwa ni jina la nchi leo hii litumike kama jina la wilaya halitaleta maana nzuri.
Meya wa Manispaa ya Mpanda Wiliy Mbogo aliomba  manispaa ya Mpanda wakabidhiwe Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  ambayo imejengwa  kwenye Manispaa  na inawahudumia zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Manispaa hiyo.
Na pamoja kuwa inawahudumia wakazi hao pia wamekuwa wakikosa nguvu za kushughulikia malalamiko ya wananchi  wanaopata huduma kwenye hospitali hiyo kwa kuwa  hawana mamlaka nayo .
Manispaa ya Mpanda inatumia kituo chake cha afya cha Mwangaza kama ndio hospitali yake ya manispaa na hawatowi huduma ya kulaza wagonjwa wanalazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo ipo katikati ya manispaa ya Mpanda.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa