Home » » ASKOFU NYAISONGA AWATAKA MADIWANI KUWAELIMISHA WATU WARAKA WA ELIMU BURE

ASKOFU NYAISONGA AWATAKA MADIWANI KUWAELIMISHA WATU WARAKA WA ELIMU BURE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter Mguluchuma
   Katavi
Askofu wa Kanisa Katoloki Jimbo la Mpanda  Gervansi Nyaisonga  amewataka madiwani wa Manispaa ya Mpanda  wasaidie  kuwaelimisha  watu  juu ya waraka  wa elmu bure  na  vipengele muhimu kwenye waraka huo  vitafusiliwe kwa lugha nyepesi.
Ushauri huo aliutowa hapo jana ofisini kwake wakati  alipokuwa akizungumza na madiwani wa Manispaa ya Mpanda walikwenda kumtembelea na kumwelezea  mikakati yao ya mipago ya maendeleo wakiongozwa na meya wa Manispaa hiyo Willy Mbogo.
Askofu Nyaisonga alisema  watu waliowengi hawauelewi waraka wa elimu bure  hivyo ni wajibu wa madiwani  kusaidia kuwaelimisha watu  waufahamu  vizuri waraka wa elimu bure.
Alieleza pamoja na kutolewa kwa waraka huo  upo umuhimu mkubwa ukatafusiliwa kwa lugha  nyepesi   hasa kwenye vipengele vile vyepesi ili wananchi wauelewe vizuri na yeye yuko tayari  kuwaelimisha waumini  wake waraka huo .
 Alisema  madiwani watambue kuwa  wao ni watu muhimu  kwenye jamii hivyo  wathamini  majukumu  yao  wajue wapo kwa ajiri ya watu  hivyo wanaowajibu  wa  kuisimamia  Manispaa yao na watu wasiende kwenye siasa ili wakaibe  .
Pia aliwataka madiwani hao wahamasishe watu  wawekeze  katika uwekezaji kwani furusa za uwekezaji   zipo nyingi  na wajitahidi kukusanya mapato yao ya ndani  kuliko kutegemea bajeti ya kutoka Serikalini  ambayo haitoshi  kuendesha shughuli za maendeleo.
Makamu wa Askofu Padri Patrick Kasoma  nchi ilikuwa na changamoto ya watu  kuwa wamekaa  bila kuwa wanafanya kazi  na walikuwa  wanajua kura tuu kuliko kufanya kazi .
Mtu  anaetaka  kuwa kiongozi  ajivue kwanza  uvivu  na ubinafsi  ndio aweze kuwaongoza watu  na madiwani wajitahidi kusimamia usafi kwani mji utakapokuwa msafi  magonjwa ya kuambukiza yatakwisha alisema Padri Kasomo.
 Alisema viongozi wengi  wamekuwa wakikosa  imani kwa wananchi  wao kwa kuwa  walikuwa  hawauziki  na walikuwa  walikuwa wakichaguliwa kwa ajiri ya fedha .
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Mpanda Wiliy Mbogo  alisema  wanalengo la kuimarisha Halmashauri yao kwa kuongeza vyanzo vyao vya ukusanyaji wa mapato .
Na swala la madiwani  kwenda kuwatembelea na kupokea maoni na ushauri kutoka kwa viongozi wa madhehebu ya dini litakuwa ni endelevu katika Manispaa ya Mpanda  kwani viongozi hao wa dini wanayo nafasi  kwenye jamii.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa