Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Watu wawili Lupimwa Julias(30) na Remi Madirisha (32) wakazi wa Kijiji cha Ilebula Tarafa ya Kabungu Wilaya ya Mpanda wamekufa hapo hapo baada ya kupigwa na radi na wengine watatu kujeruhiwa wakati wakiwa shambani.
Tukio la vifo vya watu hao wawili lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi na nusu jioni Kijijini hapo wakati watu hao wakiwa shambani kwao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia jana waandishi wa Habari kuwa watu watatu waliojeruhiwa na Radi hiyo kuwa ni Tatu Jerald ,Stela John na Filiberti Paskali wote wakazi wa Kijiji cha Ilebula Wilayani hapa.
Alisema kabla ya tukio hilo marehemu hao wawili na majeruhi walikuwa shambani kwao wakiwa wanalima shamba lao lililiopo kwenye Kijiji hicho.
Wakati wakiwa wanaendelea kulima mvua ilianza kunyesha ambapo wote waliamua kwenda kujikinga chini ya mti uliokuwa kwenye shamba lao.
Kamanda Kidavashari alieleza ndipo watu hao Radi ilipowapiga na kupelekea vifo vya watu wawili na kujeruhi watatu.
Alisema baada ya tukio majeruhi wote watatu walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na wanaendelea na matibabu katika wodi namba moja waliko lazwa huku hari zao zikiwa zinaendelea vizuri .
Na miili ya marehemu wamekabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya maandalizi ya mazishi yatakayo fanyika kesho katika makabuli ya Kijiji cha Ilebula.
Kamanda Kidavashari amewatahadharisha wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa makini katika kipindi hiki cha masika pindi mvua zinaponyesha kujihifadhi maeneo yaliosalama
0 comments:
Post a Comment