Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
MADIWANI
wa Halmashauri za Nsimbo wilaya ya Mlele na Manispaa ya mji wa Mpanda
mkoani Katavi, wameiomba Serikali kurejesha huduma ya usafiri wa abiria
kwa njia ya reli kutoka Mpanda hadi Tabora baada ya huduma hiyo
kusitishwa kwa muda sasa kutokana mafuriko yaliyotokea mkoani morogoro
hivi karibuni.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Viongozi wa Madiwani hao ambao ni Meya wa Manispaa ya mji wa Mpanda Wiliy Mbogo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,Raphael Kalinga wakiwa na Madiwani wa Kata za Katumba , Ugala na Litapunga walidai kuwa tangu kusitishwa huduma ya usafiri huo kwa abiria, wananchi wamejikuta wakikosa usafiri wa uhakika.
Meya Mbogo, alisema kwamba usafiri unaotegemewa kwa sasa ni ule wa barabara ya kutoka Mpanda kwenda tabora kupitia Inyonga yenye urefu wa kilometa 349 ambayo imekuwa ikipitika kwa shida nyakati hizi za masika ambapo kuna muda inawalazimu wasafiri kutumia saa 19 hadi 24 kutokana na sehemu nyingi kuwa korofi na magari kukwama.
Alisema imefika wakati sasa Serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana hiyo kuruhusu shirika la reli kuendelea kutoa huduma kwa abiria kwa kuwa wao hawaoni mantiki ya kuzuia njia hiyo isitumike kwa Galimoshi la abiria wakati lile la mzigo likiendelea kitumia kwa ajili ya shughuli za usafirishaji wa mizigo.
Naye, Raphael Kalinga alisema kuwa haoni sababu ya shirika la reli kuzuia safari hizo kwa treni ya abiria kwa kusingizia mafuriko ya maji yaliyotokea morogoro ambako hakuhusiani na njia ya Mpanda kwenda Tabora.
"Sasa safari za treni ya mizigo zinawezekanaje ili hali safari za abiria zishindikane?" alihoji Kalinga huku akitaka Serikali kuchukua hatua za kurejesha safari hizo, ili kuwasaidia wananchi wa ukanda huo wa magharibi wanaotegemea zaidi njia hiyo kwa usafiri wa abiria na mizigo.
Aliongeza kwamba kutokana na kukosekana kwa usafiri huo, wananchi wa vijiji vya Litapunga , Ugala , Kambuzi na Kamili wako kisiwani kwani hawana usafiri mwingine wanaoutegemea zaidi ya Treni.
Diwani wa Kata ya Ugala, Alawa Charles alisema kwa kuwa kata yake ipo mpakani mwa Mkoa wa Tabora kwa sasa wanatumia usafiri wa baiskeli umbali wa kilometa 30 kwenda Tabora kutoka na Kata hiyo kutokuwa na usafiri wa njia ya barabara.

0 comments:
Post a Comment